RAIS MAGUFULI ATOA VITAMBULISHO 670,000 KWA WAMACHINGA, AWAPA WAKUU WA MIKOA KUVITAWANYA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday, 11 December 2018

RAIS MAGUFULI ATOA VITAMBULISHO 670,000 KWA WAMACHINGA, AWAPA WAKUU WA MIKOA KUVITAWANYA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia wakati mkuu wa mkoa wa Simiyu Antony Mtaka alipokuwa akisaini hati ya makabidhiano ya vitambulisho vya wajasiriamali wadogo wadogo machinga.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizingumza na Wakuu wa Mikoa, Mawaziri na Makatibu Wakuu wa baadhi ya Wizara, Mameneja wa Mikoa wa Mamlaka ya Mapato nchini TRA, Wawakilishi wa Machinga kabla ya kutoa Vitambulisho kwa ajili ya Wafanyabiashara wadogo wadogo katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Vitambulisho hivyo vitagharimu kiasi cha Shilingi 20,000/ kwa kila kimoja.

Baadhi ya Wakuu wa Mikoa wakisikiliza hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliyokuwa akiitoa katika ukumbi wa katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia wakati Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila alipokuwa akisaini hati ya makabidhiano ya vitambulisho vya wajasiriamali wadogo wadogo machinga kwa ajili ya mkoa wa Mbeya.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipungia mkono wakati akiondoka kwenye ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa Ardhi Wiliam Lukuvi wakati akiondoka kwenye ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment