VODACOM, TECNO WAZINDUA SIMU YA TECNO CAMON 11 DAR - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday, 6 December 2018

VODACOM, TECNO WAZINDUA SIMU YA TECNO CAMON 11 DAR

 Mkuu wa kitengo cha Uhusiano na  Mawasiliano wa Vodacom Tanzania PLC, Jacquline Materu (katikati) akiwaonesha waandishi wa habari ( hawapo pichani) simu mpya  ya Tecno  aina  ya  Camon 11 na Camon 11Pro, zitakazouzwa katika maduka  ya Vodacom kwa  kiasi cha TSh. 400,000. wakati wa hafla ya  uzinduzi wa simu hizo iliyofanyika  jijini Dar es Salaam leo. Wengine wanaonesha simu hizo kutoka kushoto ni Meneja  wa Maduka ya Rejareja  ya Vodacom, Happyness  Macha na  Meneja Uhusiano wa Tecno, Erick Mkomoya.

 Wahudumu wa Vodacom wakiwa kwenye hafla hiyo.

 Mkuu wa kitengo cha Uhusiano na  Mawasiliano wa Vodacom Tanzania PLC, Jacquline Materu (wa pili kutoka kushoto) akimkabidhi simu mpya  ya Tecno  aina  ya  Camon 11 na Camon 11Pro, Mwanahabari, Goodluck Baruti baada ya kushinda bahati nasibu ya kupata simu hiyo.

 Mkuu wa kitengo cha Uhusiano na  Mawasiliano wa Vodacom Tanzania PLC, Jacquline Materu (wa pili kutoka kushoto) akimkabidhi simu mpya  ya Tecno  aina  ya  Camon 11 na Camon 11Pro, Balozi wa Tecno, Abdallah Sultani.

Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI nambari moja ya mawasiliano ya simu nchini imeungana na kampuni ya Tecno kuwaletea wateja wao toleo jipya la simu aina ya Tecno Camon 11, leo jijini Dar es Salaam. Uzinduzi huu ni harakati ya Vodacom kuhakikisha jitihada zake za kuwezesha maisha ya kidijitali kwa wateja wao, kwa kupitia simu janja zinafanikiwa.

Akizungumza na waandishi wakati wa uzinduzi wa simu hiyo, Meneja Uhusianowa kampuni ya TECNO  Bw. Eric Mkomoya alisema, “Tumedhamiria kuhakikisha kila Mtanzania anamiliki simu janja na kwa pamoja tunalifanya taifa la Tanzania kuwa la kidigitali”. 

Uzinduzi huu uliohudhuriwa na wateja lukuki utawawezesha watumiaji wa matoleo ya awali wa simu za TECNO  Camon kuweza kubadili simu zao ili kujipatia toleo hili jipya kwa kuongeza kiasi kidogo cha pesa. 

Simu hii inapatikana kwa bei ya shilingi laki nne tu (Sh. 400,000) na inakuja na Intaneti ya GB 15 ambapo mteja anapata GB tano  kwa miezi mitatu mfululizo. 

TECNO  Camon 11 ina kamera ya mbele yenye uwezo wa mega pixel 16 na kamera mbili za nyuma yenye uwezo wa mega pixel 13  na 2 kwa picha bora zaidi. Simu hii pia  inauwezo wa 4G LTE pamoja na uwezo wa kuhifadhi laini mbili za simu. Pamoja na hayo, simu hii ina flashi iliyotengenezwa kwa rangi maalumu kuweza kusaidia mwanga kutoka vizuri huku ikiwa na kioo chenye ukubwa wa inchi 6.2 chenye uwezo wa FHD. Maduka yote ya TECNO yatatoa si huduma za TECNO tu bali pia kusajili laini za Vodacom. 

“Tunafuraha kushirikiana na TECNO  kuendelea kuimarisha zaidi azimio letu la kuzidi kuwawezesha wateja wetu kuwa katika ulimwengu wa kidijitali. Uzinduzi huu umekuja katika kipindi muafaka, hasa kwakuwa Watanzania wengi zaidi wanatumia huduma za simu janja” alisema Jacquiline Materu, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania.  

Katika zama hizi za kidigitali, kupata taarifa, kununua na kulipia vitu, na kupata burudani za muziki na sinema, vinawezekana kwa kutumia simu janja, na toleo hili jipya kutoka TECNO litawezesha hayo yote na zaidi. “Uzinduzi huu umekuja sambamba na msimu wa sikukuu ili kuhakikisha wateja wetu, ambao ndiyo kipaumbele chetu wanasherehekea msimu huu kidigitali zaidi” aliongeza Materu.  

Kwa sasa, wateja wote wenye matoleo ya zamani ya TECNO Camon wanaweza kutembelea maduka ya Vodacom na TECNO  jijini Dar es Salaam, Arusha, Mwanza na mikoa mingine saba nchini ili kubadilisha simu hizo na kupata simu mpya ya TECNO Camon 11. “Nimefurahi sana kupata simu hii, nimebadilisha simu yangu ya TECNO  Camon CX na sasa nitasheherekea mwezi wa Disemba na marafiki zangu tukifurahia picha na kumbukumbu bila wasiwasi wa ubora wake. Ninawashukuru sana TECNO  na mtandao wangu wa Vodacom.” Alisema Hawa.

No comments:

Post a Comment