TANESCO YAANZA OPERESHENI KUWANASA 'WACHEPUSHA' UMEME, KADHAA WAKAMATWA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday, 17 December 2018

TANESCO YAANZA OPERESHENI KUWANASA 'WACHEPUSHA' UMEME, KADHAA WAKAMATWA

-


SHIRIKA la Umeme Nchini (TANESCO) limeanza operesheni ya na kuwanasa wachepusha umemeteja kadhaa eneo la Kinondoni Kaskazini.
Operesheni hiyo imeanza leo Desemba 17, 2018  ambapo wateja kadhaa wamebainika kufanya vitendo hivyo vya kuchepusha umeme ili usipite kwenye mita kwa ajili ya kufuatilia mwenendo wa matumizi yake na hivyo kuliibia Shirika.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari mara baada ya ukaguzi huo wa kushtukiza, Kaimu Meneja wa TANESCO anayeshughulikia wateja wakubwa, Mhandisi Frederick Njavike, alisema sio tu wateja binafsi wanaofanya hujuma hizo, lakiini pia taasisi za umma  likiwemo shirika moja la umma (jina linahifadhiwa).
Mhandisi Njavike alisema kwa kawaida kila mwisho wa mwaka Shirika hupanga siku za kufanya ukaguzi wa kushtukiza ili kuangalkia sehemu gani TANESCO inapoteza mapato “Tumekuta kuna miundombinu ya TANESCO imechezewa na mbaya zaidi ni kwamba hata taasisi za umma zinashiriki vitendo hivyo, wito wetu tunaomba taasisi zote za serikali kujaribu kupitia miundombinu yote ya umeme na vile vile kuangalia watu waliowapangisha kwenye vitegauchumi vyao.” Alisema.
Alisema TANESCO ni shirika la umma hivyo amewaomba wateja na wasio wateja kutoa taarifa kwa wale wote wanaochezea miundombinu kwani watakuwa wamesaidia shirika lao kuokoa fedha kutokana na wizi huo.
Akielezea zaidi kuhusu operesheni hiyo, Afisa wa usalama wa Shirika hilo Mkoa wa Kinondoni, Bw. Mohammed Mtoro alsiema, zipo hatua mbalimbali ambazo TANESCO huchukua dhidi ya vitendo hivyo ikiwa ni pamoja na kuwasitishgia huduma na hatua nyingine ni kufikishwa kwenye vyombo vya dola kwa hatua zaidi za kisheria.

Alisema katika ukaguzi huo wamebaini baadhi ya wateja kutengeneza njia mpya za kuingiza umeme kwenye mita zao ambapo wengine huzinyofoa kutoka kwenye mita na hivyo mita zinashindwa kurekodi matumizi halisi ya mteja huyo.Mmoja wa wateja alijitetea kuwa yeye hakujua kama kulikuwepo na udanganyifu huo kwani nyumba wanamoishi ilikuwa ya marehemu baba mkwe wake na yeye na familia yake wameanza kuishi hapo tangu mwaka 2015.

 Wataalamu wa TANESCO wakichunguza moja ya vifaa vilivyohujumiwa ili kufanya wizi wa umeme huko Mikocheni jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Meneja wa TANESCO anayeshughulikia wateja wakubwa, Mhandisi Frederick Njavike (kulia), akizunhumza jambo na Afisa Uhusiano wa TANESCO, Bi. Samia Chande, wakati wa operesheni hiyo.





No comments:

Post a Comment