Ofisa Biashara wa Benki ya NMB, Bi. Beatrice Mwambije (katikati) akiwasilisha mada kwenye kongamano la mafunzo kwa akinamama wajasiriamali 'Open Kitchen' lililodhaminiwa na Benki ya NMB. |
Ofisa Biashara wa Benki ya NMB, Bi. Beatrice Mwambije (wa kwanza kulia) akifafanua jambo juu ya huduma za NMB kwa baadhi ya washiriki kwenye kongamano la mafunzo kwa akinamama wajasiriamali 'Open Kitchen' lililodhaminiwa na Benki ya NMB.
Sehemu ya washiriki kwenye kongamano la mafunzo kwa akinamama wajasiriamali 'Open Kitchen' lililodhaminiwa na Benki ya NMB wakifuatilia mada anuai. |
Mmoja wa wafanyakazi wa Benki ya NMB (katikati aliyesimama) akigawa fomu za taarifa za NMB kwenye kongamano la mafunzo kwa akinamama wajasiriamali 'Open Kitchen' lililodhaminiwa na Benki ya NMB. |
Mwanasaikolojia Lisbeth Mhando (kulia) akiwasilisha mada kwenye kongamano la mafunzo kwa akinamama wajasiriamali 'Open Kitchen' lililodhaminiwa na Benki ya NMB. |
Mmoja wa akinamama wajasiriaamali waliofanikiwa baada ya kukuzwa na Benki ya NMB kimtaji akiwasimulia wenzake namna Benki ya NMB ilivyomsaidia kukuza biashara zake. |
BENKI ya NMB
imedhamini kongamano la mafunzo kwa akinamama wajasiriamali waliokutana jana
kupata mafunzo anuai ya kijasiriamali yaliyolenga kumuinua mwanamke kibiashara.
Kongamano hilo
lilifanyika jana jijini Dar es Salaam ambapo zaidi ya kinamama 200 kutoka
jijini Dar es Salaam na baadhi ya mikoa walinufaika na mada zilizolenga
kumnyanyua mwanamke mjasiriamali.
Akizungumza katika
kongamano hilo, Ofisa Biashara wa NMB, Bi. Beatrice Mwambije aliwataka
akinamama kujenga mazoea ya kukuza vipato vyao kwa kupunguza gharama zisizo za
msingi katika maisha.
Alisema matumizi
yasiyo ya lazima yamekuwa yakipoteza kipato cha akinamama na kujikuta
wanashindwa kukuza biashara zao, hivyo kuwashauri kuanza kubana matumizi yasiyo
ya lazima.
"...Tujifunze
kuongeza kipato chetu kwa kupunguza gharama zisizo na ulazima, tujitaahidi
kupata elimu ya kutosha hata kabla ya kuomba mkopo katika biashara zetu,"
alisema Bi. Mwambije.
Aliwashauri kuitumia
NMB katika kuendeleza biashara zao kwa mikopo kwani maofisa wa benki hiyo hutoa
elimu na ushauri wa kutosha kabla ya kumpa mkopo mfanyabiashara ili usije kuwa
mziko kipindi cha kurejesha.
Aidha aliongeza kuwa
mtaji wa biashara unaweza kuwa mali yoyote au
mali kauli kwa wajasiriamali waaminifu hivyo kuwashauri wasiogope kujitokeza
kufanya biashara kwa wale ambao bado hawajaingia rasmi kwenye biashara.
Kongamano hilo
lililokuwa na kauli mbiu; Wanawake tuna nia, tunasababu, na sasa
tunajiwezesha ambalo lilitoa nafasi kwa akinamama kupata mafunzo
toka kwa wajasiriamali waliofanikiwa ambao pia walipata fursa ya kupata mikopo inayotolewa na Benki ya NMB.
Mwanamama mjasiliamali (kushoto) akiuliza swali kwa watoa mada (hawapo pichani). |
Mwanasaikolojia Lisbeth Mhando akiwaelekeza akinamama wajasiriamali namna ya kupunguza asira au furaha iliyopitiliza kwa kutumia pumzi. |
No comments:
Post a Comment