NAIBU WAZIRI MALIASILI NA UTALII, KANYASU ATEMBELEA HIFADHI YA TAIFA RUBONDO - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday, 12 December 2018

NAIBU WAZIRI MALIASILI NA UTALII, KANYASU ATEMBELEA HIFADHI YA TAIFA RUBONDO

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu (kulia) akipewa maelezo kutoka kwa Mkuu wa Hifadhi ya Kisiwa cha Rubondo, Ignas Gara (katikati) mara baada ya kuwasili katika hifadhi ya kisiwa hicho ambapo ambapo aliweza kuzungumza na watumishi wa Hifadhi hiyo iliyopo wilayani Chato mkoani Geita. Kushoto ni Afisa wanyamapori wa Hifadhi hiyo, Emmanuel Kaaya.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu (katikati) akipewa maelezo kutoka kwa Meneja wa Hoteli ya Asilia, Adam Juma (wa pili kulia) akiwa pamoja na Mkuu wa Hifadhi hiyo, John Gara (wa pili kushoto) wakati alipofanya ziara katika hifadhi ya Taifa  ya  kisiwa cha Rubondo    ambapo aliweza kutembelea  hoteli hiyo iliyopo ndani ya  Hifadhi hiyo  iliyopo wilayani Chato mkoani Geita. Kulia ni Afisa wanyamapori wa Hifadhi hiyo, Emmanuel Kaaya na kulia ni Adrian William.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akiwa pamoja na Mkuu wa Hifadhi hiyo, John Gara (kulia) wakiangalia baadhi ya picha kwenye simu ya Sokwe wakati Naibu Waziri huyo alipofanya ziara katika hifadhi ya Taifa  ya  kisiwa cha Rubondo, Kushoto ni Katibu wa Naibu Waziri huyo,Bw. Zulu Ng’ondya.

No comments:

Post a Comment