BENKI YA NMB YATOA MSAADA WA KOMPYUTA MIKOCHENI SEKONDARI DAR - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday, 4 December 2018

BENKI YA NMB YATOA MSAADA WA KOMPYUTA MIKOCHENI SEKONDARI DAR

Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Badru Idd, akimkabidhi, Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mikocheni, Salama Ndyetabura, moja kati ya kompyuta tano zilizotolewa na benki hiyo leo hii kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi wa shule hiyo. Wa pili  kutoka kushoto ni Meneja wa benki hiyo, Tawi la Msasani, Halima Mcharazo. Wengine ni wanafunzi wa shule hiyo.

 Meneja wa benki hiyo, Tawi la Msasani, Halima Mcharazo, akizungumza kwenye hafla hiyo.

 Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mikocheni, Salama Ndyetabura, akizunguza wakati akipokea msaada huo.

 Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Badru Idd, akizungumza kwenye hafla hiyo.

 Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Badru Idd, akizungumza kwenye hafla hiyo.
.

 Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mikocheni, Salama Ndyetabura, akitoa taarifa ya shule hiyo kabla ya kupokea msaada huo.

 Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mikocheni, Salama Ndyetabura, akimkabidhi taarifa ya shule hiyo, Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Badru Idd.

 Mwanafunzi wa shule hiyo, Suleiman Khamu, akielezea teknolojia ya Tehama kupitia  kompyuta walizo kabidhiwa na benki hiyo.

 Mwanafunzi wa shule hiyo, Anwar Mohamed, akielezea teknolojia ya Tehama kupitia  kompyuta walizo kabidhiwa na benki hiyo.

Mwanafunzi wa shule hiyo, Thomson Athanas, akielezea teknolojia ya Tehama kupitia  kompyuta wazizo kabidhiwa na benki hiyo.Na 

Mwandishi Wetu

BENKI ya NMB imetoa msaada wa kompyuta tano kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi kompyuta hizo, Dar es Salaam leo, Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Badru Idd alisema kompyuta hizo zitachangia kuongeza ufanisi katika ufundishaji na ujifunzaji hasa kipindi hiki ambacho dunia inaongea zaidi juu ya sayansi na teknolojia.

"Kompyuta tunazozitoa leo hii ni sehemu ya mchango wetu kwa jamii tunaimani zitaweza kuleta matokeo chanya kwa wanafunzi hususani kwenye masomo ya Tehama" alisema Idd.

Aliongeza kuwa kompyuta hizo tano zitasaidia kuimarisha mafunzo ya Tehama shuleni hapo na kuongeza uelewa mzuri wa masomo ya Tehama kwa wanafunzi wawapo shuleni na hata baada ya kumaliza masomo yao.

Idd alisema kuwa kompyuta hizo ni sehemu ya kompyuta 150 zinazopelekwa mashuleni kwa mwaka huu ambapo pia katika Wilaya ya Same wamebahatika kupata mgao wa kompyuta tano.

Akizungumzia kuhusu benki hiyo alisema ndiyo inayoongoza nchini kwa kuwa na matawi mengi kwani ina matawi zaidi 228, ATM zaidi ya 800 nchi nzima, NMB wakala zaidi ya 6000 pamoja na idadi ya wateja zaidi ya milioni 3 idadi ambayo ni hazina kuwa ukilinganisha na benki zingine na kuwa imezifikia wilaya zote kwa asimilimia 100 pamoja na kuboresha huduma za kibenki kwa njia ya mtandao ili kufikisha huduma za kibenki kwa wananchi wengi.

Mkuu wa shule hiyo, Salama Ndyetabura akipokea msaada huo alisema kwa nyakati tofauti shule hiyo imepokea misaada mbalimbali kutoka kwa wadau wa elimu yenye thamani ya sh.milioni 108,516,780 katika kipindi cha Januari 2015 hadi Oktoba 2018.

Alisema kwa msaada huo walioupokea kutoka Benki ya NMB, umeonesha dhamira ya dhati katika kuunga mkono nia ya dhati ya Rais Dkt.John Magufuli ya kutoa elimu ya msingi bila malipo yoyote kwa watanzania.

Katika hatua nyingine Ndyetabura alisema kwamba katika kuhakikisha wanafanikiwa kitaaluma shule hiyo ilipata wafadhili ambao waliwapatia kompyupa tano na kuwaunganisha kwenye mkongo wa Taifa huduma ambayo inawawezesha kupata makala na mambo mbalimbali na kufundisha kwa njia ya mtandao ambapo ameiomba benki hiyo kuwasaidia kwa mara nyingine kupata Projekta ambayo itasaidia kufundisha wanafunzi kwa njia ya teknolojia kwa urahisi zaidi kufundisha masomo yote ambapo wataweza kutekeleza sera ya elimu ya mwaka 2007.



No comments:

Post a Comment