VIONGOZI TUGHE WATAKIWA KUWA VIELELEZO VYA UADILIFU KWENYE MAENEO YA KAZI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Friday, 23 November 2018

VIONGOZI TUGHE WATAKIWA KUWA VIELELEZO VYA UADILIFU KWENYE MAENEO YA KAZI

Halmashauri ya TUGHE ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na menejimenti ya TMA wakiwa katika vikao. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk. Agnes Kijazi akiwa katika kikao hicho.

Halmashauri ya TUGHE ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na menejimenti ya TMA wakiwa katika vikao.

Picha ya pamoja ya kikao cha Halmashauri ya TUGHE ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na menejimenti ya TMA.

HALMASHAURI
ya TUGHE ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na menejiment ya TMA wamejumuika katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa TMA makao makuu,Ubungo Plaza tarehe 22 Novemba 2018.

Katika kikao hicho, Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dk. Agnes Kijazi aliwataka viongozi wa TUGHE kuwa vielelezo vya uadilifu kwenye maeneo yao ya kazi.

Aliongezea kuwa ni vyema viongozi  wa TUGHE na menejiment ya TMA kuweka vipaumbele vya ufanisi wa kazi ili kufanikisha maendeleo ya nchi kupitia huduma za hali ya hewa zinazotolewa na TMA

Wakati huo huo alisisitiza haki iende sambamba na wajibu kwa kuzingatia utendaji kazi wa pamoja (team work)

Kwa upande wa TUGHE katibu wake,bw.Benjamin Bikulamchi alishukuru Menejiment ya TMA kwa ushirikiano uliopo baina yao pamoja na kutoa pongezi kwa kazi nzuri inayofanyika katika kuboresha maslahi ya wafanyakazi

Kikao hicho cha siku moja kilijadili masuala mbalimbali kwa manufaa ya Mamlaka kwa ujumla

No comments:

Post a Comment