VIJIJI VYOTE NCHINI KUPATIWA HUDUMA ZA MAJI SAFI - MAJALIWA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday, 19 November 2018

VIJIJI VYOTE NCHINI KUPATIWA HUDUMA ZA MAJI SAFI - MAJALIWA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akimsikiliza Mwenyekiti wa kijiji cha Mtua, wilayani Nachingwea, Anthony Makota   wakati  aliposoma taarifa kuhusu matatizo yanayokikabili kijiji hicho mbele ya   Waziri Mkuu ambaye alisimama kijijini hapo kuwasalimia wananchi, Novemba 17, 2018 . Kulia ni Mbunge wa Nachingwea, Hasan Masala.  (Picha na Ofisi ya Wazri Mkuu).

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwaamesema Serikali imedhamiria kuhakikisha wananchi wote wakiwemo wa wilaya ya Nachingwea wanapata huduma ya maji safi na salama karibu na makazi yao, hivyo amewataka wananchi waendelee kuiamini.

Ameyasema hayo Novemba 17, 2018 alipokuwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Namatula ‘A’ na kijiji cha Mtua ambao waliosimamisha msafara wa Waziri Mkuu wakati akiekea Kata ya Kilimarondo wilayani Nachingwea.

“Serikaliya Awamu ya Tano ina mikakati mizuri inayolenga kumaliza tatizo la upatikanaji wa maji safi na salama katika maeneo mbalimbali nchini vikiwemo vijiji vya wilaya ya Nachingwea ili kuwawezesha wananchi kupata huduma hiyo.”

Waziri Mkuu amesemaSerikali kupitia Kampeni ya Rais Dkt. John Magufuli ya kumtua mama ndoo, itahakikisha wananchi katika maeneo yote nchini wanapata huduma ya maji safi na salama karibu na maeneo yao ya makazi.

Amesema mbali na huduma ya maji, pia Serikali imedhamiria kusambaza umeme katika vijiji vyote ambavyo bado havijaunganishiwa nishati hiyo nchini vitaunganishiwa katika awamu ya tatu ya Mradi wa Nishati Vijijini (REA).

“Rais wetu Dkt. John Magufuli anataka kuona kila nyumba ya Mtanzania inapata umeme tena kwa gharama nafuu, hivyo ametenga fedha nyingi zitakazotosheleza kusambaza umeme katika vijiji vyote vikiwemo na wilaya ya Nachingwea. Gharama za kuunganishiwa umeme huo ni sh. 27,000 tu.”

Pia Waziri Mkuu ameesema wananchi hawatowajibika tena katika kulipia gharama za nguzo wala fomu za maombi ya kuunganishiwa umeme, kwa sababu tayari gharama hizo zimeshabebwa na Serikali.

Awali, Waziri Mkuu alimkabidhi Mwenyekiti wa kijiji cha Mpiluka saruji tani mbili na nusu kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya shule ya Msingi Mpiluka.

No comments:

Post a Comment