RAIS WA ZANZIBAR AFANYA MAZUNGUMZO NA JUMUIYA YA KAUNTI ZA PWANI, KENYA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday, 28 November 2018

RAIS WA ZANZIBAR AFANYA MAZUNGUMZO NA JUMUIYA YA KAUNTI ZA PWANI, KENYA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza wakati wa mkutano wa pamoja na Jumuiya za Kaunti za Pwani Nchini Kenya mkutano uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Inter Continental Jijini Nairobi, kushoto Balozi wa Kenya Nchini Tanzania Mhe. Dan Kazungu.(Picha na Ikulu).

Mshauri wa Rais wa Zanzibar Masualia ya Ushirikiano wa Kimataifa Uchumi na Fedha Balozi Mohammed Ramia, akichangia wakati wa mkutano huo na Jumuiya ya Kaunti ya Pwani Nchini Kenya, uliozikutanisha pande hizo mbili kuzungumzia changamoto za uvuvi. mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa hoteli ya Inter Continental Jijini Nairobi Kenya.(Picha na Ikulu).

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Balozi wa Kenya Nchini Tanzania Balozi Dan Kazungu, akiutambulisha Ujumbe wa Magavana wa Jumuiya ya Kaunti za Pwani, wakati wa mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Inter Continental Jijini Nairobi kuzungumzia changamoto zinazowakabili Wananchi wa pande hizo mbili.(Picha Ikulu).

Gavana wa Kaunti ya Mombasa Mhe. Hassan Ali Joho, akichangia wakati wa Mkutano huo wa pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, kuzungumzia changamoto za pande mbili hizi, katika masuala ya uvuvi, zilizokutanisha Ujumbe wa Tanzania na Jumuiya ya Kaunti za Pwani Nchini Kenya, mkutano uliofanyika ukumbi wa hoteli ya Inter Continental Jijini Nairobi.(Picha na Ikulu).

No comments:

Post a Comment