Wafanyakazi wa vodacom kitengo cha IT na M-Pesa wakipeana chenga kwenye viwanja vya Gymkhana wakati wa maadhimisho ya Vodacom Sports Bonanza jijini Dar es salaam jana. |
Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakishindana mchezo wa kuogelea jana katika viwanja vya Gymkhana wakati wa maadhimisho ya Vodacom Sports Bonanaza. |
KAMPUNI ya mawasiliano Vodacom Tanzania imehimiza
wafanyakazi wake pamoja na jamii kuzingatia michezo ili kuweza kuimarisha
utendaji kazi pamoja na ubora wa afya kwa manufaa binafsi na manufaa ya taifa
kwa ujumla.
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Kitengo cha Usalama
wa Kazi Vodacom, Bi. Karen Lwakatare wakati wa siku ya ‘Vodacom Sport Bonanza Day’
iliyofanyika katika uwanja wa Gymkhana Dar es Salaam.
"Tunafanya bonanza kwa ajili ya
wafanyakazi wote wa Vodacom kuhamasisha mazoezi kwa afya ya wafanyakazi na jamii
kiujumla.
Mshindi atakayepatikana anapata fursa ya
kwenda kushiriki mashindano ya Vodacom Wellbeing Challenge ya mwaka ambayo
hufanyika nje ya nchi, yanayo wakutanisha wafanyakazi wa Vodacom na Vodafone
duniani,” Lwakatare aliongeza.
Bonaza hilo limehusisha michezo ya aina
mbalimbali ikiwa ni pamoja na mpira wa miguu, kukimbia, kuogelea, gofu, tenesi,
Volley ball, kuruka kamba, draft, rede kutembea kwa miguu na kuendesha
baisikeli kutoka ofisi za makao makuu ya Vodacom hadi Gymkhana.
Mfanyakazi wa Vodacom akiwaongoza wenzake katika mchezo wa kuendesha baisikeli kutoka makao makuu ya ofisi za Vodacom hadi viwanja vya Gymkhana jana wakati wa maadhimisho ya Vodacom Sports Bonanza jijini Dar es Salaam.
Sandra Oswald, mfanyakazi wa Vodacom akicheza mchezo wa gofu katika viwanja vya Gymkhana jana wakati wa maadhimisho ya Vodacom Sports Bonanza jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa kampuni ya Vodacom wakifanya mazoezi ya viungo jana katika viwanja vya Gymkhana kuadhimisha siku ya Vodacom Sports Bonanza. |
Mwanandada Naaja akiwaongoza wafanya kazi wa Vodacom Tanzania kwenye mazoezi ya viungo jana katika viwanja vya Gymkhana. |
No comments:
Post a Comment