UKANDAMIZAJI KWENYE JAMII UNAZUIA WASICHANA KUTUMIA SIMU - UTAFITI WA KIMATAIFA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday, 17 October 2018

UKANDAMIZAJI KWENYE JAMII UNAZUIA WASICHANA KUTUMIA SIMU - UTAFITI WA KIMATAIFA



UKANDAMIZAJI KWENYE JAMII UNAZUIA WASICHANA KUTUMIA SIMU - UTAFITI WA KIMATAIFA

SIKU ya binti, Asasi isiyo ya kibiashara ya Girl Effect ikishirikiana na Vodafone Foundation leo imechapisha matokeo ya utafiti wa kwanza wa kimataifa juu ya jinsi wasichana wadogo wanavyopata na kutumia teknolojia ya simu. 

Utafiti unaonesha kwamba wavulana wana uwezekano wa kuwa na simu mara 1.5 zaidi kuliko wasichana, na kuwa na uwezekano wa kuwa na simu janja (Smart phone) mara 1.3 zaidi , kutokana na  upendeleo wa kijamii na vikwazo vingine vyenye kuzuia matumizi ya simu kwa wasichana.

Uhuru wa kutumia simu za mkononi kwa wasichana walio katika nchi zinazoendelea ni mdogo kuliko inavyotarajiwa; wakati 44% tu ya wasichana waliohojiwa katika utafiti walisema wanamiliki simu, zaidi ya nusu (52%) walisema wanapata simu kwa kuazima.

Hata hivyo, utafiti unaonesha kwamba simu zinafanya wasichana kujisikia kutotengwa(50%), kuwa na uhuru wa kupata  elimu (47%), kujiburudisha (62%), kuwafunulia habari zilizofichika(26%), na kuwafanya wajiamini (20%).

Tunaunganishwa na dunia, tunawezeshwa kujua zaidi kuhusu yale tunayojifunza, na kujifunza mambo mengine mengi kupitia mtandao. Tunaweza kujua kuhusu mambo tusiyoyajua. (Msichana, 19, Bangladesh)

Hata hivyo, utafiti huu – wa ubora na uwiano, uliofanyika katika nchi 25 - umegundua kuwa uhuru wa  matumizi ya simu kwa wasichana unadhibitiwa  kwa kiasi kikubwa na mazoea ya kijamii ambayo huwazuia kuwa na uhuru sawa na wavulana. Zaidi ya theluthi mbili (67%) ya wavulana waliohusishwa kwenye utafiti waliripoti kuwa na simu (ikilinganishwa na 44% ya wasichana) na 28% wakisema waliazima - ikilinganishwa na zaidi ya nusu (52%) kwa wasichana.

Aidha, katika nchi kama Nigeria, Malawi na Tanzania, wavulana wana uwezekano mkubwa wa kutumia simu kwa shughuli nyingi zaidi kama Whatsapp na Facebook, kutafuta habari kwa mtandao, au kutafuta kazikuliko wasichana. Katika maeneo haya, wasichana, kwa upande mwingine, hutumia simu kwa kazi za kawaida zenye kuhitaji ujuzi na ufahamu mdogo sana, mathalan kuwapigiawazazi wao au kutumia kikokoteo.

Katika nchi kama India na Bangladesh, wasichana wanaoonekana kutumia simu, mara nyingi hutazamwa vibaya na wanajamii, kwa maana wazazi wana uwezekano mkubwa zaidi wa kupiga marufuku matumizi ya simu. Wasichana ambao huvunja sheria zihusianazo na simu pia wana uwezekano mkubwa wa kuadhibiwa kwa kukemewa, kupigwa, kufukuzwa shule au hata kufungishwa ndoa mapema.

Ikiwa ni msichana mwenye umri wa miaka 15, hawezi kuruhusiwa kuondoka nyumbani kwake, atapigwa na kunyang’anywa nafasi yake ya kutwaa  elimu.  Pia inaweza kutokea akaozeshwa. (Msichana, 17, India)

Vikwazo juu ya matumizi ya simu kwa wasichana pia inamaanisha wasichana wanaweza kutumia njia zisizo salama na za siri ili kupata simu. Katika maeneo kama Nigeria ya Kaskazini, ambapo wasichana wanahitaji idhini ya wazazi kutumia simu, wasichana wanasema kwamba wavulana mara nyingi huwapa wasichana wao simu za siri, ili waweze kuwasiliana nao kwa faragha kila wanapohitaji.

Matokeo yake, wasichana wanaona hofu ya wazazi juu ya usalama wao ndio kizuizi kikuu kwaokupata simu (47%), ambapo wavulana wanasema gharama ndio kizuizi kikubwa zaidi (60%).

Kecia Bertermann, Mkurugenzi wa ufundi na Utafiti wa kidijitali, Girl Effect, alisema: "Upatikanaji sawa wa teknolojia ni eneo la utafiti lenye kukua, lakini 'wasichana' hupatikana mara kwa mara ndani ya jamii kubwa ya 'wanawake' na hivyo changamoto ambazo ni mahususi kwao huwa haziripotiwi. Utafiti huu unaonyesha ukweli wa hali halisi ya wasichana walivyo nyuma kwenye foleni ya kupata simu.

Hii ina maana wasichana hupata matatizo zaidi na manufaa kidogo kama yapo;  bila kupewa muda au idhini ya kujiamini kudadisi matumizi makubwa zaidi ya simu elimu na ujuzi wa kiteknolojia wa wasichana hudumazwa. Pili, kwa kuwa wasichana wengine wanaamua kutumia  simu kwa siri, wanaweza kuogopa kutoa taarifa kwa wazazi au marafiki pale ambapo kuna jambo hatarishi, na hivyo kujiweka kwenye hatari kubwa zaidi. "
Malawi na Rwanda ambako upatikanaji wa simu ni mdogo na ujuzi wa wasichana wa teknolojia ni mdogo zaidi, hata wasichana wenyewe wanaogopa kwamba simu zinaweza kuwasababisha 'kupotea' kutokana na  kuwasiliana na wavulana jambo ambalo hatimaye, linaweza kupelekea kupatikana kwa mimba zisizohitajika.

Wengine wanaamini kwamba mvulana na msichana ni watu tofauti, wengine wanasema kwamba mvulana anaweza kuwa na simu wakati wowote wakati msichana akiwa na simu anaweza kuishia kupata ujauzito. (Msichana, 19, Malawi)

Hata hivyo, wasichana wote kiujumla wanaona kwamba kuwa na simu ya mkononi kunaweza kuwasaidia kuwa salama zaidi. Wasichana wanasisitiza zaidi kuliko wavulana jinsi simu inavyoweza kuwa muhimu katika kupunguza hali hatarishi katika maisha yao. Mara nyingi hoja hii hutolewa kama kigezo cha msingi kwaokutaka kuruhusiwa kumiliki simu katika nchi ambazo wasichana wachache zaidi huwa na simu na kuwa na matumizi madogo zaidi.

Andrew Dunnett, Mkurugenzi wa Vodafone Foundation, alisema: "Wasichana wanaachwa nyuma. Katika nchi nyingi upatikanaji wa simu ni muhimu kwa elimu, maendeleo na afya ya wasichana. Tunahitaji kukabiliana na ukweli kwamba wasichana na wavulana hawana uhuru sawa wa kupata simunahuduma za kiubunifu mahususi kwa ajili ya wasichana ili kukidhi mahitaji yao katika muktadha huu.

Tunataka utafiti huu ujulishe pamoja na kuunga mkono sekta za teknolojia na maendeleo katika kukidhi mahitaji ya wasichana ili kuleta maendeleo ya ukweli katika jitihada zetu za kufikia Malengo ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo. "

Vodafone Foundation wakishirikiananaGirl Effect wamedhamiria kuwawezesha wasichana milioni saba katika nchi nane walioathirika na upatikanaji wa huduma wanazohitaji kupitia simu. Wakishirikiana na washirika na wafadhili wengine wengi, lengo likiwa ni kukusanya fedha zinazofikia hadi jumla ya $ 25m katika kipindi cha miaka mitano, ikiwa ni pamoja na mchango wa $ 5m kutoka kwa Vodafone Foundation ili kufikia malengo haya makubwa.

Utafiti huu ambao ni wa kwanza wa aina yake, unawahimiza viongozi katika tasnia za maendeleo na tekinolojia  kutambua vikwazo vya kijamii vinavyokwaza wasichana kuwa na uhuru wa kutumia simu za mkononi. Vodafone Foundation naGirl Effect wanatoa wito kwa tasnia kuchukua hatua na kufanya yafuatayo:

MANIFESTO YA VODAFONE FOUNDATION NA GIRL EFFECT
JUU YA WASICHANA NA SIMU ZA MKONONI

1. Kabili pengo lote la kijinsia kwenye matumizi ya simu za mkononi.Wasichana wanakabiliwa na vizuizi vya kimwili vinavyowazuia kupata simu za mkononi, lakini mara nyingi ni vikwazo vya kijamii ambavyo ni vigumu zaidi kuvuka. Hivi vinaweza kushughulikiwa kwa ufanisi kwa kuzingatia mazingira ya ndani na kuchukua mbinu timilifu, ili kuweza kukabiliana na vikwazo vingi kwa wakati mmoja kupitia njia zakidijitali na zisizo zakidijitali.

2. Badili kiwango cha ufahamu kwa ajili ya zama za kidijitali. Ufahamu wa tekinolojia ni sehemu muhimu ya elimu - wasichana wana hatari ya kurudi nyuma ikiwa hatuwekezi katika hili. Msaada unapaswa kuhusisha kuunganisha ufahamu wa tekinolojia na usalama wa kidijitali katika mifumo ya ufundishaji kwa ajili ya wanafunzi wote, pamoja na wazazi na jamii kuruhusu zaidi matumizi ya  simu za mkononi.

3. Ubunifu kwa ajili ya usalama mtandaoni - Wasichana kila mahali - kutoka Nigeria ya kaskazini hadi kata ya Adams, Colorado - wanataka matumizi yao mtandaoni kuwa salama zaidi. Wakati wa kubuni majukwaa ya kidijitali, tunapaswa kuwafikiria  watumiaji wanaoazima simu.
Tunahitaji kubuni mazingira yaliyo salama kwa msichana ambaye ana tumia vifaa mbali mbali katika vipindi tofauti, kama ilivyo kwa binti mwenye uhuru na kifaa au simu yake mwenyewe.

4. Husisha wanaume na wavulana. Wanaume na wavulana mara nyingi hupata simu za mkononi kwa urahisi zaidi kuliko wasichana na wanawake, na wakati mwingine huwa kama ukuta baina ya simu za mkononi na wasichana au wanawake. Tunahitaji kusaidia wanaume na wavulana hawa katika kukabili vikwazo vya kijamii vinavyozunguka matumizi ya simu za mkononi na kuonyesha jinsi simu hizi zilivyo na manufaa katika maisha ya wasichana.

5. Wasaidie wasichana kukuza upeo wao wa kidigitali na kushiriki katika ubunifu. Wasichana wako kwenye nafasi nzuri zaidi ya watu wenginekufumbua matatizo yanayowakabili katika maisha yao. Hii inatoa fursa kubwa kwa sekta ya teknolojia kuingiza wasichana katika mchakato wa maendeleo. Tunahitaji kuongeza ufahamu wa teknolojia kwa wasichana - kutoka kwenye matumizi ya kawaida ya simu, kwenda kwenye kuandika programu za kompyuta zenye ubunifu na ufumbuzi wa maswala mbali mbali yanayowahusu - na kuwezesha uhuru huu kuchochea ubunifu na uvumbuzi usio na mipaka.

No comments:

Post a Comment