HDIECA NA MAONESHO YA WAJASILIAMALI KUONESHA KAZI ZA MIKONO - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday, 9 October 2018

HDIECA NA MAONESHO YA WAJASILIAMALI KUONESHA KAZI ZA MIKONO

TAASISI ya isiyo ya Kiserikali inayojishughulisha na maswala ya Mazingira pamoja na Utu (HDIECA), iliandaa maonesho maalum ambayo yaliwakutanisha wajasiliamali mbalimbali ambao wanafanya shughuli zao kwa kutumia mikono yao kwa lengo la kurudisha shukurani zao kwa  jamii kutokana na wananchi kupokea na kushirikiana nao vyema katika kazi zao mbalimbali wanazozifanya kila siku.

Maonesho hayo yalifanyika katika viwanja vya Azura Kawe Jijini Dar es Salaam na hakukuwa na kiingilio chochote kwa wananchi na wajasiliamali hawakulipia kitu ilikuwa ni Bure kabisa.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wajasiliamali wengi waliishukuru taasisi hivyo kwa kuwapa fursa hiyo hata ya kuonesha kazi zao na kufahamiana na watumbalimbali na pia kuongeza wigo wa kibiashara kwa kupata wateja wapya.

Baadhi ya wadau mbalimbali wakiwa wanatazama bidhaa  za wajasiliamali.

Mmoja wa wajasiliamali (aliyevaa T-shirt nyeupe) akitoa maelezo ya namna dawa zake za asili zinazofanya kazi.

Mkurugenzi wa Taasisi ya HDIECA Bi. Sarah Pima (aliyevaa kofia) akiwa katika moja ya banda la mjasiliamali kuangalia bidhaa ya unga wa lishe wakati wa maonesho hayo.

Mmoja wa wajasiliamali (anayenyoosha kidole) akimpa maelekezo mgeni aliyetembelea banda hilo kuhusiana na kazi zao za sanaa wanazozifanya ikiwa ni pamoja na kuchora.

Mmoja wa wajasiliamali (aliyevaa ushungi) akiwa anamuuzia mteja Juice zake ambapo moja ya Juice iliyokuwapo ni ya Mapalachichi.

 Katika maonesho hayo kulikuwa na wajasiliamali wanaotengeneza vitu mbalimbali kwa mikono yao ambapo pamoja na yote waliomba ikiwezekana watengewe sehemu ambayo watakuwa wanapeleka bidhaa zao na kuziuza hata mara moja kwa mwezi.

Wananchi wakiendelea kutazama Bidhaa mbalimbali zilizotengenezwa na watanzania.

 Wa kwanza kulia ni Dada mbunifu ambaye yeye anabadili matairi chakavu kuwa mapambo na vitu kw ajili ya matumizi mbali mbali, mfano hawa wadau walio kaa ukiacha (aliyevaa kofia ya njano) vimetengenezwa kwa mataili, vitu hivyo walivyo kalia unaweza weka viatu, Nguo za watoto, kuna stuli za kukalia pia.

Watu wakendelea kutazama bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na watanzania.

 Wajasiliamali mbalimbali pamoja na waandaaji wa maonesho hayo wakiwa katika picha ya pamoja.

 Moja ya Banda la mjasiliamali anayetengeneza Batiki.

  Moja ya Banda la mjasiliamali anayetumia chupa chakavu zilizotupwa anaokota na kuziongezea thamani kwa kuviwekea marembo kwa kutumia nyuzi vitambaa na nakshi nakshi zengine.

  Moja ya Banda la mjasiliamali anayetengeneza bidhaa zao kwa kutumia mishumaa na maua ya asili.

  Moja ya Banda la mjasiliamali anayetengeneza Bangiri, Hereni, Cheni na vitu mbalimbali kwa kutumia Shanga.

  Moja ya Banda la mjasiliamali anayetengeneza Note Book kwa kuvalishia kava la kitenge.

 Mjasiliamali anayeuza Ubuyu wa nazi.

  Moja ya Banda la mjasiliamali anayetengeneza mafuta ya aina mbalimbali.

  Moja ya Banda la mjasiliamali anayetengeneza mapambo mbalimbali kwa kutumia kamba na misumali.

Haya hapa chini yote ni matairi, mjasiliamali huyu anayaongezea thamani yanakuwa  kama yanavyo onekana hapa.

Aliyevaa kofia ya njano anaitwa Bw. Nzowa yeye baada ya kusikia kuwa kutakuwa na wajasilamali wanafanya maonesho yao na yeye akaja na Gereji yake inayotembea kwa lengo la kuona kama anaweza kupata fursa na kutengeneza Magari lakini pia kutoa elimu ya namna gereji ya kutembea inavyofanya kazi.

Picha zote na Fredy Njeje

No comments:

Post a Comment