TWENDE: SHULE YA UVUMBUZI TANZANIA INAYOTUMIA BAISKELI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday, 24 July 2018

TWENDE: SHULE YA UVUMBUZI TANZANIA INAYOTUMIA BAISKELI

Frank Molle anasema kuwa likwama yake ya kusambaza mbolea ni mfano mzuri wa aina ya uvumbuzi wa teknolojia unaohitajika barani Afrika kila siku.

Uvumbuzi mwingine.

BERNARD Kiwia anaweza kutengeza chochote kutoka kwa baiskeli.
Mara ya kwanza alijulikana kwa kuvumbua chaja ya simu inayotumia nguvu za baiskeli.
Bernard alianza kazi kama fundi wa baiskeli hadi alipogundua kwamba anaweza kutengeza vitu vingi zaidi kutokana na vipuri vya baiskeli . Alianza uvumbuzi na hajawacha.
''Nabuni teknolojia kwasababu nimegundua kwamba ni kitu ambacho kinaweza kuisaidia familia yangu na jamii'', alisema Bernard.
Mashine ya kuosha nguo inayoendeshwa na kibaramwezi inaokoa wakati na juhudi za familia yake kwa kuwa huosha nguo wakati upepo unapokuwa mwingi.
Uvumbuzi wa Bernard sasa umeenea kutoka nyumbani kwake hadi kwa jamii yake.
Takriban wavumbuzi 800 kutoka nchini humo walitumia karakana ya uvumbuzi alioanzisha kwa jina Twende.
Anaitwa baba wa uvumbuzi wa mashambani nchini Tanzania
Kile tunachotaka kuwaonyesha watu ni kwamba wana ujuzi kunazisha teknolojia zao ambazo wanaweza kuzimudu, wanazoweza kurekebisha, na kupata vipuri wanavyohitaji, alisema Bernard.
Watu wanaoishi mashambani hupta mapato ya chini mara kwa mara na mashine zinazonunuliwa dukani hawawezi kuzinunua kwasababu ni ghali mno. Hii ndio sababu kwamba naangazia mashine za mashambani.
Mmoja wa wavumbuzi hao ni Frank Molle ambaye alivumbua Fert-Cart-likwama inayosaidia kupunguza muda mwingi unaotumiwa kusambaza mbolea katika mashamba kwa kutumia mikono.
Biashara ya Frank inashirikisha likwama inayoweza kukodishiwa wakulima ambao hawana ardhi ya kutosha na faida ili kuweza kununua uvumbuzi wake.
Twende inahakikisha kwamba wale wote waliopo katika warsha yao wanajifunza mikakati ya biashara nzuri na ,mipango ya biashara
Mmoja wa wateja wake anasema kuwa utumizi wa mashine hiyo kumemsaidia kuwa na uwezo wa kuwalipia wanawe karo za shule
''Likwama hupunguza mabilioni ya saa ambayo hupotea katika shughuli za kilimo, alisema Frank. Afrika hususan nchini Tanzania , inahitaji ubunifu wa teknolojia ya riwaya ambayo inaweza kusaidia wakulima kuongeza uzalishaji wao wa mazao na mapato miongoni mwa wakulima wadogo. "

Kifaa cha kukamua mafuta ya avocado cha Jesse Oljienge tayari kinabadilisha maisha ya jami.
"Twende ni ubunifu wa kijamii ," Kulingana na Jesse. "kuna watu wanaofanya miradi tofauti katika chumba kimoja. Kwa hivyo iwapo una tatizo unaweza kuzungumza na mtu yeyote kwenye meza na utapata suluhisho."
Kabla ya uvumbuzi huo wa kukamua mafuta katika ovakado, bidhaa hiyo ingeweza kuoza inapoanguka kwa sababu wakulima hawakuweza kupata bei nzuri katika soko. Sasa wanawake katika jamii hutumia kifaa hicho kutoa mafuta wanaoyouza sokoni.
Jesse anasema kwamba ushirikiano wake na Twende umemsaidia kutuma maombi ya kupata ufadhili wakitumia karakakan hiyo kama shirika. Ufadhili na kupata mtaji ni miongoni mwa changamoto mbili zinazowakabili wawekezaji wa nchini.
Zaidi ya yote kuwa na mshauri kama Bernard husaidia.
''Iwapo una tatizo na huwezi kupata suluhu , mwambie Bernard, yeye hufikiria kwa dakika mbili na atakwambia tumia njia hii''. .Hivyobasi tunapata ushauri mwingi, anasema Jesse.
Maisha ya Magreth Shemkaye yamebadilishwa na mashine aliyotengeneza Twende ili kukata sabuni.

Imemfanya kuanza biashara yake ya sabuni mbali na kuwasaidia wanawake wengine katika mji wake ambao ni wajane, ili hata wao nao wapate kipato.
Nashukuru kwamba watoto wangu hawafukuzwi shule kutokana na kutolipa karo za shule, anasema. Ni mfano ambapo ubunifu unaweza kubadilisha maisha ya wengi

"Ndoto yangu ya siku zijazo ni kuona Watanzania na bidhaa zao wenyewe, vifaa vinavyoweza kutusaidia na shughuli zetu za kila siku." Bernard anasema.
Ili kuhakikisha kuwa hilo linafanyika huwaalika watoto wa shule kutoka eneo hilo kwenda Twende kuhamasisha uvumbuzi wa kisasa.. Warsha hiyo pia ina gari dogo ambalo hutumika kwenda vijijini na vifaa na mafunzo.
"Katika Twende tunafanya uumbaji ambao utasaidia jamii. Kwa hiyo tunaona changamoto inayoathiri jamii na kujaribu kukabiliana nayo ili kutatua shida hiyo," anasema Mwanafunzi Lightness Simon Mwanga Simon Kinisa.
Pamoja na masomo katika ujuzi wa vitendo kama uchomeleaji, programu ya shule ya Twende pia inajumuisha warsha kuhusu jinsi ya kuendesha biashara ndogo na kutekeleza bajeti.
"Bernard Kiwia ni mtu maalum sana." anasema Issa Kanguni kutoka kwa Wabunifu wa Tanzania na shirika la wavumbuzi wakuu.
Ni vigumu sana kuwa mvumbuzi wa Afrika au Tanzania kwa sababu wale ambao wana mawazo ya ubunifu hawana uwezo. "Anasema.
Kwa kugawana rasilimali katika Twende, Bernard Kiwia anatumai kuhamasisha jamii yake kuendelea kuwa wabunifu kwa hali na mali na kutoa suluhu zitakazo wasaidia wengine duniani .
Mara nyengine unafeli, hivyobasi unalazimika kujaribu tena ,Bernard anasema. Mara nyengine unafeli tena,hivuobasi unafanya tena, na mwisho unapofanikiwa unapata kitu kizuri.

No comments:

Post a Comment