𝗝𝗞𝗖𝗜-𝗔𝗟𝗠𝗖 𝗡𝗔 𝗚𝗦𝗠 𝗙𝗢𝗨𝗡𝗗𝗔𝗧𝗜𝗢𝗡 𝗪𝗔𝗣𝗢𝗡𝗚𝗘𝗭𝗪𝗔 𝗞𝗨𝗘𝗡𝗗𝗘𝗦𝗛𝗔 𝗞𝗔𝗠𝗕𝗜 𝗬𝗔 𝗠𝗔𝗧𝗜𝗕𝗔𝗕𝗨 𝗠𝗞𝗢𝗔𝗡𝗜 𝗔𝗥𝗨𝗦𝗛𝗔 - THE HABARII

THE HABARII

HABARI | MATUKIO | MICHEZO.


ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday, 1 September 2026

𝗝𝗞𝗖𝗜-𝗔𝗟𝗠𝗖 𝗡𝗔 𝗚𝗦𝗠 𝗙𝗢𝗨𝗡𝗗𝗔𝗧𝗜𝗢𝗡 𝗪𝗔𝗣𝗢𝗡𝗚𝗘𝗭𝗪𝗔 𝗞𝗨𝗘𝗡𝗗𝗘𝗦𝗛𝗔 𝗞𝗔𝗠𝗕𝗜 𝗬𝗔 𝗠𝗔𝗧𝗜𝗕𝗔𝗕𝗨 𝗠𝗞𝗢𝗔𝗡𝗜 𝗔𝗥𝗨𝗦𝗛𝗔

Na Mwandishi Maalumu – Arusha

WANANCHI wa mkoa wa Arusha wameipongeza Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete – Hospitali ya Arusha Lutheran Medical Centre (JKCI-ALMC) kwa kushirikiana na Kampuni ya GSM Foundation kuendesha kambi maalumu ya uchunguzi na matibabu ya magonjwa yasiyoambukiza mkoani humo.

Pongezi hizo zimetolewa na wananchi waliojitokeza kufanya uchunguzi wa afya katika kambi hiyo inayofanyika katika viwanja vya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete–Hospitali ya Arusha Lutheran Medical Centre (JKCI–ALMC) iliyopo jijini Arusha.

Wananchi hao walisema kupitia kambi hiyo wameweza kupata fursa ya kufanya uchunguzi wa afya, kujua namba zao pamoja na ushauri kutoka kwa watalamu wa afya bila

Aisha Juma mkazi wa Arusha alisema mbali na wananchi kupata huduma za afya na ushauri kutoka kwa wataalamu wa JKCI-ALMC wataalamu hao pia wamekuwa wakiwasaidia wanaichi hao kupata huduma nyingine za jamii kama vile kuwapa viburudisho, kuwasaidia kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine wale wasiojiweza na kuchukua mawasiliano yao kwaajili ya ufuatiliaji wa hali zao.

“Afya ni bora kuliko pesa, watu wakilijua hili wataona umuhimu wa kufanya uchunguzi wa afya kuliko kuhangaika na kutafuta pesa kwasababu pesa tunazozitafuta hapo baadaye zinaweza kutumika hadi kuisha kwa kutafuta huduma za afya”, alisema Aisha

Naye mkazi wa Arusha mjini John Matemu alisema amefika katika Hospitali hiyo mara baada ya kupata taarifa hivyo akaona ni muhimu kufika na kufanya uchunguzi wa aya ya macho yake kutokana na alivyokuwa akijisikia.

“Huduma ni nzuri na tunazipata kwa wakati, watu wengi wakipata taarifa ya kambi za matibabu wanahofia muda kutokana na idadi kubwa ya wanaohitaji huduma hizi, lakini hapa wameweka utaratibu mzuri ambao unarahisisha upatikanaji wa huduma kwa wakati”, alisema John

No comments:

Post a Comment