BENKI ya NMB imekabidhi jezi zenye thamani ya Shilingi milioni 36 kwa Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (Shimiwi), ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za kukuza michezo miongoni mwa watumishi wa umma nchini.
Hafla ya makabidhiano hayo imefanyika jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi wa Shimiwi wakiongozwa na Katibu Mkuu Alex Temba na Naibu Katibu Mkuu Mariam Kihange. Akizungumza katika hafla hiyo, Meneja Mwandamizi wa Idara ya Mahusiano ya Benki ya NMB na Serikali, Amanda Feruzi, alisema benki inaona michezo kama chachu ya mshikamano, afya bora na kuongeza ari ya utendaji kazi kwa watumishi.
Katika makabidhiano hayo, NMB ilikabidhi jezi, tracksuit na kombe kwa uongozi wa Shimiwi, ikiwa ni maandalizi ya michezo inayowakutanisha Wizara na Idara za Serikali. Viongozi wa NMB walioungana na Feruzi katika tukio hilo ni Meneja NMB Kenyatta Deogratius Kawoga na Meneja Mahusiano Mwandamizi wa NMB, Josephine Kulwa.







No comments:
Post a Comment