NMB YADHAMINI NA KUSHIRIKI KIKAO KAZI CHA WENYEVITI WA BODI NA WAKUU TAASISI ZA UMMA - THE HABARII

THE HABARII

HABARI | MATUKIO | MICHEZO.


ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday, 26 August 2025

NMB YADHAMINI NA KUSHIRIKI KIKAO KAZI CHA WENYEVITI WA BODI NA WAKUU TAASISI ZA UMMA







BENKI ya NMB imedhamini na kushiriki kwenye Kikao kazi cha wenyeviti wa Bodi na watendaji wakuu wa taasisi za umma (CEOs Forum.

2025) kinachoendelea katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano Arusha (Arusha International Conference Centre).

Ujumbe wa NMB umeongozwa na David Nchimbi - Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi pamoja na Juma Kimori - Afisa Mkuu wa Fedha na Kaimu Afisa Mtendaji mkuu.

Kikao kazi hicho cha Siku tatu kinawashirikisha Viongozi zaidi ya Mia Sita Hamsini kutoka Taasisi, Mashirika na Wakala wa Serikali. Kauli mbiu ya Kikao hicho ni “Kujenga Ushirikiano Endelevu katika Mazingira ya Ushindani wa Kimataifa – Wajibu wa Mashirika ya Umma.

No comments:

Post a Comment