MAPINDUZI MAKUBWA SEKTA YA UJENZI NCHINI YAJA...! - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Friday, 18 July 2025

MAPINDUZI MAKUBWA SEKTA YA UJENZI NCHINI YAJA...!

Msimamizi wa masuala ya sheria na miongozo wa Yusra Ltd, Deborah Joseph akizungumza na Mwandishi wa Habari hizi Dunstan Mhilu katika viwanja vya maonesho vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam.

Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Yusra Ltd, Sheikh Mohamed I . Hemed akizungumza na Mwandishi wa Habari hizi katika maonesho hayo yanayoendelea viwanja vya Mnazi mmoja Dar es Salaam.
NA DUNSTAN MHILU

SEKTA ya ujenzi na wapenda maendeleo kwa ujumla watarajie mapinduzi makubwa katika sekta ya ujenzi nchini, ambapo Shilingi bilioni 80.85 zitawekezwa nchini katika ujenzi wa nyumba 97,000, ambapo Dodoma ni nyumba 67,000 na Zanzibar 12,000.

Mikataba ya ujenzi wa nyumba hizo unatokana na uwekezaji mkubwa wa kiwanda cha bidhaa za ujenzi na teknolojia yake hapa nchini, ambapo kitajengwa katika kijiji cha Pigo, kata ya Pera wilayani Chalinze mkoani pwani katika robo ya kwanza 2026.

Hayo yamesemwa jana na, Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi ya Kifedha  Yusra Sukuk Ltd , Sheikh Mohamed I. Hemed alipozungumza katika maonesho ya ‘’Muharam Expo 2025 1447 H’’ yanayoendelea katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.

Sheikh Hemed amesema kwamba mapinduzi hayo makubwa yanayofanyika nchini yanafanyika Kwa sababu mbalimbali, lakini zipo ambazo ni kivutio kwa wawekezaji wa kubwa kuwekeza nchini hususani wawekezaji wakigeni.

“Kuna mambo ambayo hataukatae ukweli utabaki palepale, Tanzania tunasonga mbele kwasababu ya utulivu wa amani iliyopo , sinabudi kumpa kongole Rais Dk. Samia Suluhu Hassan na wasaidizi wake wote wa dola na mihimili yote mitatu” alisema Sheikh Hemed.

Sheikh Hemed amesema watu wanaweza wasielewe, pasina shaka taasisi zianzotoa mikopo au kufanya uwekezaji pasipo kutoza riba , zina mchango mkubwa katika Taifa hili. Ndiyo maana baadhi ya wawekezaji wengi huwekeza katika Taasisi zisizo toza riba ikiwemo Kampuni ya Yusra Sukuk Ltd ambayo ipo katika mstari wa mbele kuwasaidia wawekezaji wa ndani na wakimataifa.

Aidha Sheikh Hemed ameeleza faida za ujenzi wa Kiwanda hicho ambapo kina teknolojia za kisasa na ambapo nyumba ya skwea mita 2,200 za mraba hujengwa kwa siku moja na skwea mita kama hizo za ghorofa pia kwa siku moja huku ghorofa za skwea mita hizohizo hujengwa kwa siku moja pia na ghorofa ya dali kumi likijengwa kwa siku saba.

 “Ni jinsi gani mwekezaji huyu kutoka Ujerumani amejidhatiti katika teknolojia na kama hiyo haitoshi tofali lake moja lina Kg 1.4 wakati tofali la kawaida hapa nchini lina Kg 13.6-Kg 15.9 “Haya ni mapinduzi makubwa katika ujenzi na Sukuk Ltd inajivunia kuwa sehemu na mdau mkubwa katika mradi huo,“ alitanabaisha Sheikh Hemed.

Pamoja na maelezo hayo, msimamizi wa masuala ya sheria na miongozo ya Yusra Sukuk, Deborah Joseph amewaomba wananchikuzuru katika banda lao katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam wawzekuelimika na masuala mbalimbali ya hati fungani.

“Watakapotembelea banda letu watakutana na wataalamu wabobezi kuhusu masuala ya uwekezaji hususani uwekezaji usio kuwa na riba lakini pia milango ya ofisi zetu katika jengo la RITA ghorofa ya 3 ipo wazi wakati wowote wa saa za kazi jumatatu hadi Ijumaa” amesema Deborah.

No comments:

Post a Comment