Na Dotto Mwaibale, Dar es Salaam
KIJANA na mdau wa mazingira Shukuru Shahibu Selemani (35)
ametangaza nia ya kugombea Udiwani Kata ya Ligoma Wilaya ya Tunduru mkoani
Ruvuma kupitia Chama Cha Mapinzuzi (CCM), ili kupambana na Diwani aliyemaliza muda wake, Abdallah
Zuberi Mmara ambaye ametangaza kutetea nafasi hiyo.
Wagombea wengine ambao wanatajwa kuwania nafasi hiyo ni
Ahusi Manganya, Juma Jasi na Daud Likwata wote wakiwa wakazi wa kata hiyo ya
Ligoma.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam, Juni 25, 2025, Shukuru alisema ameonesha nia ya kugombea nafasi hiyo kwa lengo la kuchochea
maendeleo zaidi kwenye kata hiyo kutokana na kuwa na uwezo.
“Ni ukweli usiopingika kwamba Serikali chini ya Rais Dkt. Samia
Suluhu Hassan imefanya maendeleo makubwa katika kata yetu tunamshukuru sana
mama yetu na nimeamua kugombea nafasi hii ili kuongeza kasi ya maendelea
kuanzia pale alipoichia diwani aliyemaliza muda wake ndugu Abdallah Mmara,”
alisema Shukuru.
Shukuru alisema anagombea nafasi hiyo kupitia CCM kwa mara
ya pili na awamu ya kwanza aligombea kupitia Chama cha Wananchi CUF kabla ya
kuhamia chama tawala.
Alisema kwa mara ya kwanza kugombea nafasi hiyo kuptia CCM katika
mchakato wa kura za maoni hazikutosha
ambapo alishika nafasi ya pili akiongoza diwani ambaye amemaliza muda wake
hatua ambayo inampa matumaini makubwa ya kushinda awamu hii.
Shukuru Shahibu Selemani ni mtaalamu wa usafi wa mazingira
mwenye taasisi inayotoa mafunzo na kuhamasisha utunzaji wa mazingira katika shule mbalimbali nchini.
Pamoja na kujishughulisha na kazi hiyo pia
anajishughulisha na uchimbaji mdogo wa madini ambapo anashirikiana na vijana
kutoka maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Tunduru hasa katika kata hiyo akiwa kiongozi wao.

No comments:
Post a Comment