Naibu Katibu Wizara ya Ujenzi, Dkt. Charles Msonde akizungumza alipokuwa akifungua semina ya siku mbili ya Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi kuhusu mafunzo endelevu jijini Dar es salaam leo.
| Sehemu ya wadau wakishiriki semina ya siku mbili ya Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi kuhusu mafunzo endelevu jijini Dar es salaam leo. |
| Sehemu ya wadau wakishiriki semina ya siku mbili ya Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi kuhusu mafunzo endelevu jijini Dar es salaam leo. |
NAIBU Katibu Wizara ya Ujenzi Dkt. Charles Msonde amezungumzia umuhimu wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi nchini (AQRB), kujitangaza ili huduma zao zitumiwe na wananchi wengi.
Akifungua semina ya siku
mbili ya Wabunifu Majengo na Wakadiriaji
Majenzi kuhusu mafunzo endelevu jijini Dar es salaam leo Dkt. Msonde amesema
Serikali itaendelea kuiunga mkono AQRB ili isimamie kikamilifu sekta hiyo na
hivyo kuleta tija na ustawi kwa wananchi na sekta ya majenzi kwa ujumla.
"Kazi ya kuelimisha
wananchi iwe endelevu ili wananchi wengi wajenge nyumba za kisasa na bora kwa
gharama nafuu", amesema Dkt. Msonde.
Naibu Katibu Mkuu Msonde
amehimiza matumizi ya TEHAMA katika sekta ya majenzi ili kuendana na mabadiliko
ya sayansi na teknolojia.
Amesema Serikali
itaendelea kutumia wataalam wazawa katika miradi mingi hivyo unganeni ili mpate
fursa ya kupata miradi itakayowawezesha kukuza ujuzi na uchumi wa wataalam na
kampuni kwa ujumla.
"Tuwe na dhamira ya
kujiendeleza kiujuzi, weledi, uadilifu na uzalendo ili kufikia malengo",
amesisitiza Dkt. Msonde.
Ameitaka AQRB kufanya
tafiti ili kupata wataalam na kuwasajili kwa wakati, kuendeleza programu za
mafunzo ili kuendana na wakati, kushiriki miradi ya ndani na nje ya nchi na
kuzingatia sheria na kanuni zinazosimamia sekta ya majenzi nchini.
Naye Kaimu Msajili AQRB
Arch.Dkt. Daniel Matondo amesema semina hiyo ina lengo la kuwaweka wataalam wa
majenzi pamoja kujadili na kubuni ufumbuzi utakaowezesha sekta ya majenzi
kuendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia.
Amesema mafunzo hayo
yanayoongozwa na kauli mbiu kujenga utaalam endelevu viwango na mikakati
yanakusudia kuhamasisha Serikali na jamii kutoa kipaumbele kwa fani za ubunifu
majengo na ukadiriaji majenzi kwa ustawi wa nchi.
Kwa upande wake Msajili
wa Bodi ya Wahandisi, Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi Zanzibar Arch.
Yasir De Costa amezungumzia umuhimu wa wataalam hao Kutoka pande zote za
Muungano kushirikiana na kusaini mikataba itakayowawezesha kufanyakazi kwa
umoja na kunufaika na fursa zilizopo nchini.
Zaidi kampuni 491 na
wataalam 1707 wabunifu majengo na wakadiriaji majenzi wamesajiliwa na AQRB
kufanya shughuli za majenzi nchini kote.

No comments:
Post a Comment