![]() |
| Kaimu Naibu Mkuu wa Chuo Taaluma,Utafiti, Machapisho na ushauri elekezi Dk, Eva Luhwavi. |
![]() |
| Baadhi ya wanafunzi wa chuo cha NIT wakimsikiliza muwezeshaji wa semina hiyo hayupo pichani |
CHUO cha Usafirishaji (NIT) kimeendelea kuwapiga msasa wanafunzi wake ili kukabiliana na changamoto za ajira baada baada ya kuhitimu masomo yao.
Hayo yamejiri katika ukumbi wa chuo hicho kilichopo Mabibo Mkoani Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wanafunzi wa mwaka wa tatu wa chuo hicho kutoka kozi mbalimbali zitolewazo chuoni hapo.
Akizungumza wakati wa semina hiyo ya siku moja iliyoandaliwa na NIT, Kaimu Naibu Mkuu wa Chuo (Taaluma Utafiti Machapisho na Ushauri Elekezi) Dk, Eva Luhwavi amesema ni utaratibu wao wa kawaida kuwajengea uwezo wanafunzi wa chuo hicho wamakaribia kuhitimu masomo yao.
“NIT imekuwa na utaratibu wa aina hii kwa muda mrefu sasa lengo nikuhakikisha wanafunzi wetu wanapotoka wasiwe wageni sana katika masuala ya ajira wajipange kikamilifu na kile wanachokwenda kukumbana nacho katika soko la ajira” amesema.
Aidha Dk, Eva amesema pamoja na kuwanoa ipaswavyo katika ujuzi wanafunzi katika eneo la ujuzi na maarifa hutumia jukwaa hilo kwakuwaunganisha na wahitimu wa miaka ya nyuma waliopitia chuo hicho kwakubadirisha uzoefu siku chache kabla ya mahafali (Convocation).
Vilevile chuo hicho huandaa mitaala ya kozi za usafirishaji kwakushirikiana na wadau waliopo katika tasnia ya usafirishaji ambao muda wote wanashughulika na usafirishaji hivyo wanajua soko la sekta hiyo linahitaji nini.
Kwa upande wao wanafunzi wa chuo hicho wakizungumza na TheHabarii wameushukuru uongozi wa chuo kwakuwa na utamaduni huo ambao huwanoa katika eneo la uzoefu na wanapoingia katika soko la ajira wanjua baadhi ya vitu tofauti na wale ambao hawajajengewa uwezo.
“Naitwa Neema Fabian mwanafunzi wa mwaka wa tatu nasoma kozi ya Rasilimali watu , mafunzo haya ni muhimu kwetu na yamekuja wakati muafaka ambapo yametufumbua mambo mbalimbali kama ujuavyo chuoni tunakomaa na madesa tu ili tusifeli kumbe kuna maisha baada ya madesa tutayatumia mafunzo haya katika tasnia zetu huko tuendako” amesema.
Naye John Fabiani mwanafunzi wa mwaka watatu kozi ya Uhusiano wa Umma na masoko amesema amejifunza vitu vingi ambavyo alikuwa akiviona ni vya kawaida kumbe vina kanuni na miiko yake.
“Mfano mzuri hata kuandika barua ya maombi ya kazi n ahata kuandaa CV kunahitaji umakini na siyo kukurupuka CV nzuri na barua nzuri husaidia Zaidi kujiuza katika ulimwengu wa ajira na kumvutia mwaajiri aweze kukuajiri” amesema Fabian.




No comments:
Post a Comment