MNEKI AMPA KONGOLE SAMIA KWA KAZI YA KUTUKUKA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Sunday, 18 May 2025

MNEKI AMPA KONGOLE SAMIA KWA KAZI YA KUTUKUKA

p> 
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM,Mkoa wa Dar es Salaam,wilaya ya Kigamboni, Haran Sanga akizungumza na wananchi wakati wa kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa 2024.

Na Dunstan Mhilu

MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (MNEKI) Mkoa wa Dar es Salaam,anayewakilisha wilaya ya Kigamboni, Haran Nyakisa Sanga amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk, Samia Suluhu Hassan anastahili pongezi na heshima kwa kazi ya kutukuka aliyoitendea taifa na watanzania kwa miaka minne ya uongozi wake.

Ameyasema hayo leo ofisini kwake akiongea na mwandishi wa habari hizi katika mahojiano maalumu kuhusu tathimini yake ya miaka minne ya Rais katika Nyanja mbalimbali hususani katika halmashauri ya Kigamboni mkoani Dar es Salaam.

“Kimsingi, Rais na Mama yetu kipenzi Dk, Samia Suluhu Hassan ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Taifa na Amiri Jeshi Mkuu wa Tanzania anastahili maua yake kwa namna anavyoendesha nchi na chama. “ Nayasema haya kwakuwa katika chama ametutendea makubwa na kurahisisha shughuli za kisiasa kwakutupatia vitendea kazi kama magari, pikipiki na sasa baiskeli kwa ajili ya wajumbe wa mashina zinakuja nani kama mama Samia Suluhu Hassan” amesema Sanga.

Kando ya mchango wake katika chama, Sanga amesema kimaendeleo mama amefanya makubwa kwa taifa kwakuendeleza miradi iliyoachwa na mtangulizi wake na ile aliyoibuni ,vyote vikifanikiwa kwa asilimia kubwa jambo ambalo Sanga anamuona Dk Samia kama Rais Jabali, nguli na shupavu.

“Pamoja na kutekeleza miradi mbalimbali kwa vitendo Rais Samia ametuheshimisha wanakigamboni kwakutujengea barabara ya kiwango cha lami ya Kilometa 85 kutoka Feri-Pemba mnazi-Tundwisongani, kukamilika kwa barabara hii kutakuza uchumi wa halmashauri hiyo na kuchagiza uchumi wa kaya na taifa kwa ujumla” amesema Sanga.

Akizungumzia khali ya kisiasa ndani CCM, Sanga amesema ,chini ya uongozi wa Dk, Samia kuna utulivu na nidhamu ya hali ya juu ambapo kanuni na katiba ya CCM vinaheshimiwa na wanachama wanaheshimiana na pia amepongeza mabadiliko ya kanuni za uchaguzi katika chama hicho yaliyoafikiwa hivi karibuni na mkutano mkuu wa namna yakutafuta mgombea wa udiwani na ubunge ambapo majina yote huchujwa na kurejeshwa majina matatu na kisha kumpata mgombea mmoja.

Vilevile amesema kuwepo kwa ukomo wa viti maalumu na ubunge wa jimbo ni jambo muhimu kwakuwa lengo la viti maalumu ni kulelewa ili ukuwe ukishakuwa unatakiwa ujitegemee na kwa jimbo vivyo hivyo huwezi kuwa mbunge wa umilele kwakufanya hivyo huleta chachu ya maendeleo.

Wananchi wa Kkigamboni na wana CCM wakimsikiliza Mjumbe wa Halmashauri kuu mkoa wa Dar es Salaam, Haran Sanga wakati  wa kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa 2024.

Mjumbe huyo ambaye aliwahi kugombea ubunge katika jimbo la Kigamboni 2020 nakushika nafasi ya nne kwa kura 15 amesema hadi sasa hawezi kusema kwamba atagombea au laa kwakua Mwenyekiti alishatoa maagizo yakutofanya uchaguzi kabla ya muda muafaka hivyo ibaki tu kwamba wakati ukifika itajulikana.

“ Wakati ukifika nitatamka kwamba nimo ama simo lakini kwakuwa baadhi ya changamoto zilizoacha nitie nia bado hazijaisha huenda dhamira ikaniladhimu nifanye hivyo lakini kwa sasa yatosha kusema kwamba tusubiri wakati” amesema Sanga.

Wito wake kwa vijana ,wajitume nakufanya kazi kwa bidii, wawe wabunifu na waendane na matumizi ya tehama kwani maendeleo yanahitaji kasi ya hali ya juu na kasi hiyo muarobaini wake ni Tehama ambayo hurahisisha mambo.

No comments:

Post a Comment