MAFUNZO YA UJASIRIAMALI NA STADI ZA BIASHARA KWA WAFUNGWA YAZINDULIWA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday, 7 May 2025

MAFUNZO YA UJASIRIAMALI NA STADI ZA BIASHARA KWA WAFUNGWA YAZINDULIWA

CHUO cha Uhasibu Arusha (IAA) kwa kushirikiana na Jeshi la Magereza Tanzania wamezindua rasmi programu ya mafunzo ya ujasiriamali na stadi za biashara kwa wafungwa, ikiwa ni hatua ya kuimarisha juhudi za urekebishaji. Uzinduzi huo umefanyika leo Mei 6, 2025, na yameanza na wafungwa 40 katika Gereza Kuu la Arusha.

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, CGP Jeremiah Katungu, ameipongeza IAA kwa utekelezaji wa haraka tangu kusainiwa kwa makubaliano ya ushirikiano mnamo Septemba 2024.

Kwa upande wake, Mkuu wa Chuo - IAA, Prof. Eliamani Sedoyeka, amesema mafunzo hayo ni mwanzo wa mpango mpana wa kuwajengea wafungwa ujuzi endelevu wa maisha, ikiwemo kozi za udereva na elimu ya ngazi ya juu.

No comments:

Post a Comment