MWENYEKITI wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameweka jiwe la msingi la jengo la ofisi ya Makao Makuu ya CCM jijini Dodoma leo tarehe 28 Mei 2025.
Akizungumza na maelfu ya Wananchi ambao wamejitokeza katika hafla hiyo amesema tukio hilo limebeba mambo makubwa mawili muhimu kwa Chama cha Mapinduzi.
Mosi amesema linaakisi ndoto ya Waasisi wa CCM wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kwanza wa CCM, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na pili linathibitisha umadhubuti wa kupanga na kuamua na kutenda mambo makubwa yenye maslahi kwa Chama na Taifa letu.
"Nina amini baada ya kukamilika kwa jengo hili sio tu litatumika kwa kazi za utawala bali litakuwa alama isiyofutika isiyofutika ya uimara, umoja na utambulisho wa CCM ndani na nje ya nchi. Tutakuwa na jengo ka kisasa linaloakisi sio ukubwa wa Chama chetu bali pia nafasi ya Chama hichi kuongoza Tanzania na kuwa Chama kikubwa Afrika haswa kusini mwa bara la Afrika," amesema Dkt. Samia.
Dkt. Samia amemnukuu pia mmoja wa Waasisi wa Tanzania na aliyekuwa Rais wa ASP na Rais wa kwanza wa Zanzibar, Hayati Aman Abeid Karume aliposema ili Chama kisimame lazima watu wakione, wakisikie na wakiheshimu.
"Naomba kuwasisitiza viongozi na watendaji wa CCM haswa Vijana utendaji mzuri wa Chama sio kuwa na jengo la fahari bali utendaji mzuri wa Chama tunayoijenga na zile za mikoa na wilaya ni sehemu wanachama wetu hususani vijana watapata nafasi ya kupatumia ili kujifunza na kujijenga kiuongozi na kimaadili pia mahala pa mikutano, mijadala, tafiti, mafunzo na maamuzi ya kisera, tukahakikishe Chama chetu kinazidi kuonekana, kusikika na kuheshimika," amesema Dkt. Samia
Aidha amekumbushia kuhusu Ilani ya Uchaguzi inawataka CCM kuwa daraja la Wananchi na Serikali hivyo amewataka viongozi kutumia ofisi hizo kufikisha kero za wananchi Serikalini ili ziweze kupatiwa ufumbuzi.


No comments:
Post a Comment