DKT. NCHEMBA ATOA WITO KWA NCHI ZA AFRIKA KUHIMIZA MATUMIZA YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday 19 September 2024

DKT. NCHEMBA ATOA WITO KWA NCHI ZA AFRIKA KUHIMIZA MATUMIZA YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (kushoto), akiwa na Rais wa Madagascar, Mhe. Andry Rajoelina, (Katikati) na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Africa50, Dkt. Adesina Akwinumi, baada ya kuhutubia wakati wa ufunguzi wa  Mkutano ya Mwaka wa Wanahisa wa Taasisi ya Africa50 (General Shareholders Meeting - GSM) na Jukwaa la Miundombinu la Afrika (Infra for Africa Forum meeting) ambalo Tanzania ni mwanachama, uliofanyika tarehe 19 Septemba, 2024, Antananarivo nchini Madagascar. Mhe. efDkt. Nchemba amemwakilisha Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika Mkutano huo.

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (kushoto), akihutubia kwaniaba ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwenye Mkutano ya Mwaka wa Wanahisa wa Taasisi ya Africa50 (General Shareholders Meeting - GSM) na Jukwaa la Miundombinu la Afrika (Infra for Africa Forum meeting) ambalo Tanzania ni mwanachama, uliofanyika  tarehe 19 Septemba, 2024, Mjini Antananarivo nchini Madagascar.

Na Benny Mwaipaja

WAZIRI wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba ((Mb), ametoa wito kwa nchi za Afrika kutafuta njia na mikakati ya kuboresha uchumi na maisha ya wananchi wake kwa kutumia nishati safi ya kupikia ikiwa ni hatua pia ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya Tabianchi yanayochangiwa na uharibifu wa mazingira.

Dkt. Nchemba ametoa wito huo mjini Antananarivo  nchini Madagascar kwa niaba ya Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati akihutubia katika Mkutano wa Mwaka wa Wanahisa wa Taasisi ya Africa50 (General Shareholders Meeting - GSM) na Jukwaa la Miundombinu la Afrika (Infra for Africa Forum meeting) Taasisi ambayo Tanzania ni mwanachama, uliofanyika leo tarehe 19 Septemba, 2024, katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Ivato, na kufunguliwa na Rais wa Nchi hiyo, Mhe. Andry Rajoelina.

Aidha, Dkt. Nchemba alizishauri nchi hizo kuwekeza katika kutoa elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa wananchi wao kutumia nishati safi ya kupikia pamoja na faida zinazoambatana na utunzaji wa mazingira kiuchumi na kijamii.

Dkt. Nchemba pia ametoa wito kwa taasisi za fedha na sekta binafsi kushiriki katika kampeni ya matumizi ya Nishati safi ya kupikia ikiwemo gesi iliyosindwa, Nishati ya jua, umeme wa joto ardhi, biogas, kwa kuwezesha upatikanaji wa fedha na pia kuzalisha vifaa ama majiko yanayotumia nishati hiyo.

Katika msafara huo, Mhe. Dkt. Nchemba ameambatana na Naibu Katibu Mkuu anayesimamia Fedha za Umma (Public Finance Management) Bi. Amina Khamis Shaaban na Balozi wa Tanzania nchini Madagascar, Mwenye makazi, Maputo nchini Msumbiji, Mhe. Faustine Kasike.

Mkutano wa Wanahisa wa Africa50, unatarajiwa kuwakutanisha wadau mbalimbali kutoka Bara la Afrika na duniani kwa ujumla wakiwemo Wawekezaji kutoka Taasisi za Umma na Sekta Binafsi, wakopeshaji, wataalam wa ujenzi wa miundombinu na kuwawezesha kutafuta suluhisho la changamoto za miundombinu katika Bara la Afrika pamoja na kukabikliana na athari za mabadiliko ya tabianchi na watahimizana kuhusu matumizi ya nishati safai ili kuchochea uchumi na maendeleo ya nchi hizo.

No comments:

Post a Comment