DKT. NATU AKUTANA NA UJUMBE WA IMF, WB NA COMSEC - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Friday 27 September 2024

DKT. NATU AKUTANA NA UJUMBE WA IMF, WB NA COMSEC

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (kulia) akiagana na Naibu Mkuu Divisheni, Divisheni ya Fedha za Serikali, Idara ya Takwimu, Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Bw. Andrew Kitili, baada ya kikao cha kufunga zoezi la kutathmini ubora wa Takwimu za Madeni ya Sekta ya Umma (PSDS), kilichofanyika Jijini Dodoma.

Naibu Mkuu Divisheni, Divisheni ya Fedha za Serikali, Idara ya Takwimu, Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Bw. Andrew Kitili, akizungumza wakati wa kikao na katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha ambapo aliishukuru Serikali ya Tanzania kwa kutoa ushirikiano wakati wakifanya tathmini ubora wa Takwimu za Madeni ya Sekta ya Umma (PSDS), kilichofanyika jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, akiongoza mkutano na Ujumbe wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Benki ya Dunia (WB) na Sekretarieti ya Jumuiya ya Madola (COMSEC), kwa ajili ya kufunga zoezi la kutathmini ubora wa Takwimu za Madeni ya Sekta ya Umma (PSDS), kilichofanyika Jijini Dodoma.

Na Asia Singano, WF, Dodoma

KATIBU Mkuu, Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El maamry Mwamba, amekutana na Ujumbe wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Benki ya Dunia (WB) na Sekretarieti ya Jumuiya ya Madola (COMSEC), kwa ajili ya kufunga zoezi la kutathmini ubora wa Takwimu za Madeni ya Sekta ya Umma (PSDS), nchini Tanzania.

Zoezi hilo lilifanywa kuanzia tarehe 23 hadi 27 Septemba 2024 ambapo ujumbe huo ulikutana na Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Wizara mbalimbali na Taasisi za Serikali ambapo pamoja na mambo mengine tathmini hiyo ililenga kuangalia na kubaini ubora na mapungufu yaliyopo katika ukusanyaji, uchakataji na usambazaji wa takwimu hizo.

No comments:

Post a Comment