Meneja Mradi wa EMEDO, Bw. Arthur Mugema akionesha moja ya kifaa okozi aina ya boya (life Jacket) kwenye warsha hiyo kwa wanahabari. |
Mchambuzi mwandamizi wa Hali ya Hewa kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), akiwasilisha mada katika warsha hiyo. |
Baadhi ya washiriki wa warsha hiyo wakifuatilia mada. |
Ofisa Uhusiano wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), Bi. Monica Mutoni akizungumza katika warsha hiyo. |
Na Joachim Mushi, Dar
SHIRIKA lisilokuwa la kiserikali la usimamizi wa Mazingira na Maendeleo ya Uchumi (EMEDO), linalofanya shughuli zake Ziwa Victoria limetoa warsha kwa wanahabari juu ya tahadhari zinazotakiwa kuchukuliwa na watumiaji wa fursa za majini hasa kwa wavuvi ili kupunguza ajali wawapo katika shughuli zao za uvuvi.
Akizungumza alipokuwa akiwasilisha mada, Meneja Mradi wa EMEDO, Arthur Mugema ameshauri watumiaji wa shughuli za uvuvi baharini, katika mito na maziwa hasa wavuvi kuhakikisha wanakuwa na vifaa maalumu vya kuwasaidia wapatapo na ajali za majini kama vile maboya okozi (life Jacket).
Alishauri Serikali kuangalia uwezekano wa kupunguza kodi kwa vifaa okozi majini yakiwemo maboya ya kufaliwa na wavuvi wawapo katika shughuli za uvuvi majini (Life Jacket) kwani kwa sasa bei zake zipo juu jambo ambalo, linachangia wwengi kushindwa gharama zake nao kushindwa kuyatumia.
Mbali na kuomba wadau kuzidisha kutoa elimu kwa umuhimu wa vifaa hivyo okozi kwa watumiaji wote wa vyombo vya majini, zoezi hilo linapaswa kwenda pamoja na upunguzaji wa kodi ili viweze kupatikana kila mahali na kwa bei nafuu, kuchochea matumizi ya wengi kwa watumiaji.
Hata hivyo, alisema, mwaka 2021 walifanya utafiti wa ajali nyingi za wavuvi kuzama ziwani na kubaini kuwa licha ya uelewa hafifu juu ya matumizi ya vifaa vya uokoaji pia kundi hilo halipati taarifa za hali ya hewa kwa wakati jambo ambalo lingesaidia kupungua kwa matukio ya ajali.
"Tulibaini kuwa wavuvi wanauelewa mdogo kwenye elimu ya usalama kwe ye Mji, matumizi ya vifaa maalum kama maboya okozi ni wavuvi wachache wanaotumia, japokuwa ipo sheria inaowataka wavae,...lakini hata hivyo changamoto nyingine ni upatikanaji wa maboya okozi pamoja na gharama zake kwani zimekuwa kubwa," alisema.
Akizungumza awali, Mkurugenzi wa Shirika hilo, Bi. Editruda Lukanga alisema ipo haja ya kushirikiana kwa pamoja ili kutoa elimu ambayo itasaidia kuzuia watu hasa wavuvi kufa maji wawapo katika shughuli zao.
Amesema katika ripoti ya WHO inaonyesha asilimia 90 ya vifo hivyo vinatokea katika nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania hivyo ni wakati muafaka kwa Tanzania pia kuchukua hatua hususani katika kipindi hiki ambacho mabadiliko ya hali ya hewa yamekuwa yakitokea.
"Ni wakati sasa wa kuleta mabadiliko na kuchangia usalama wa namna tunavyotumia maji," Amesema.
Naye, Ofisa Uhusiano wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), Bi. Monica Mutoni amesema wanashirikiana vizuri na EMEDO na wadau wengine ili kuzuia watu kupata na changamoto anuai za mabadiliko ya Hali ya hewa, hasa ukizingatia kuwa watu wanaofanya shughuli zao katika maziwa makuu na ukanda wa bahari wanakumbana na athari za Hali mbaya ya hewa hususani upepo mkali.
"Kama mnavyofahamu TMA sisi jukumu letu ni kutoa taarifa za hali ya hewa na hali ya hewa upande wa sekta ya uvavi hivyo tutaendelea kushirikiana na EMEDO na wadau wengine kuhakikisha kuwa taarifa hizo zinawafikia wavavi," alisema.
No comments:
Post a Comment