WAMACHINGA Kariokoo wametisha ndivyo unavyoweza kusema kwa lugha ya Kiswahili cha kisasa, ikiwa ni wiki moja tokea iweke uongozi wake mpya Madaraka ambao viongozi wa awali wote wamerudi kutokana na kazi nzuri waliyoifanya kwa takribani miaka saba sasa wamelamba dume kutoka maendeleo Benki.
Chama hicho cha wamachinga Kariakoo, (Kawaso) kimesainishiana hati ya makubaliano na kuzindua Mradi wa Ujenzi na Nyumba za Makazi kwa Wamachinga wa Dar es Salaam wenye thamani ya shilingi milioni 500, na kuwanufaisha wafanyabiashara 500.
Benki hiyo Kupitia Mkurugenzi Mtendaji wake Dk, Ibrahm Mwangalaba amesema hatua hiyo imefikiwa na Benki hiyo kutokana na kupokea maombi kutoka Kawaso kwa muda mrefu na kwakuwa ni wateja wao waaminifu hawakuwa na hiyana yakuwanyima mkopo.
“Wamachinga watakopeshwa kiasi cha Sh 1, 000,000 kwa kila mmoja kwa awamu ya kwanza na kuanza kujenga nyumba zao ili waepukane na Maisha ya kupanga” amesema Mwangalaba wakati akizungumza na Thehabarii blog
Dk, Mwangalaba amesema awamu ya pili watatoa mkopo mwingine sasa kwa ajili ya ujenzi wa makazi ya kudumu ambapo huu wa sasa ni wakununulia viwanja pekee.Aidha amesema mradi huo unajulikana kwa jina la Machinga Plot Finance.
Mwangalaba amesema mwaka 2021, benki hiyo ilianzisha utaratibu wa kuwasaidia wafanyabiashara ndogo ndogo, wa Soko la Kariakoo na masoko mengine yaliyopo Mkoa wa Dar es Salaam.
Aidha Mkurugenzi huyo amesema walengwa wa kuu wa mradi huo uliotiwa saini hii leo ni pamoja wafanyabiashara wadogo ambao wanatambuliwa na kuidhinishwa na Serikali kufanya biashara katika maeneo ya masoko maarufu kwa jina na vizimba.
Akifafanua zaidi, Dk, Mwangalaba amesema katika kipindi cha miaka 3 na nusu Maendeleo Benki imeweza kutoa kiasi cha billion 9.8 kwa wamachinga wapatao7,000 ambapo hadi sasa kiasi cha Billioni 7.5 zimeisharejeshwa na bilioni 2.3 zikiwa bado zipo mikononi mwa wafanyabiashara hao ambao wanaendelea kulipa vizuri.
Awali amesema baada ya kupitia kwa makini maombi ya ya KAWASSO, kuhusu ujenzi wa nyumba za makazi kwa wamachinga ambapo wamekubaliana kununua viwanja hivyo.
Wakati huo huo,, Mkurugenzi huyo ametaja eneo la mradi huo nakudai kuwa hadi sasa tayari wameshapata zaidi ya hekali 89, katika Kijiji cha Magoza kilichopo Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.
Mwangalaba ameendelea kusema ilikufanikisha lengo hilo, Tayari Benki hiyo ikishirikiana na KAWASSO wameingia makubaliano na kampuni ya Urasilimishaji Ardhi ya SEMSIC LAND CONSULTANT LIMITED, ambapo mpango huo utawawezesha Wamachinga wa MKOA WA Dar es Salaam kupata viwanja kwa bei ya Shilingi Mil 1 kwa kiwanja kimoja, huku wakitakiwa kuresha kidogo kidogo kwa muda wa miezi 12.
Vilevile Mkurugenzi huyo amesema wao kama Maendeleo Benki wakitambua Jitiahada zinazofanywa na Serikali ili kukuza Uchumi na kupunguza umaskini Serikali haiwezi kufanikiwa bila kushirikiana na Sekta Binafsi hivyo na wao wameona Bora waunge mkoano jitiahada hizo.
Kaimu Mwenyekiti wa KAWASSO, Namoto Yussuf Namoto.Kwa upande wake, amesema wao wameishukuru benki hiyo kwa kitendo cha kuunga mkono juhudi zao ambapo Leo historia imeandikwa katika kufanikisha kutiwa Saini kwa mkataba wa Ujenzi na Utekelezwaji wa Mradi huo amesema Namoto.
“Historia kweli imeandikwa niwaahidi wamachinga wenzanu, kwamba watuamini kama viongozi wao tumedhamiria kuwavusha na waachane na porojo za wasiyowatakia wamachinga mema ni wakati wawamachinga kuheshimika na tumeahidi kufanya kazi usiku na mchana kuhakikisha mmachinga anapata haki zake stahiki katika Taifa lao mama” amesema
Vilevile amewaomba wamachinga ambao hawajajiunga na chama hivyo wajiunge ili washikamane na wanufaike na fursa mbalimbali za kiuchumi.
“Mimi na Mwenyekiti wangu na wajumbe wote tuliochaguliwa hivi karibuni katu na kamwe hatuwezi kuwa wachoyo kwa fursa yoyote inayokuja mbele yetu hivyo ambao hawajajiunga hawajachelewa hata leo milango ipo wazi na yajayo yanafurahisha.

No comments:
Post a Comment