![]() |
Muonekano wa barabara
ya Lindi – Dar es Salaam eneo la Somanga ambalo zoezi la urejeshaji wa
miundombinu ya barabara hiyo imeimarishwa, Mkoani Lindi.
![]() |
Waziri wa Ujenzi,
Innocent Bashungwa akimsikiliza Mkazi wa eneo la Mikereng’ende, Shaweji
Kibwebwe wakati alipokuwa akisimamia zoezi la urejeshaji wa
miundombinu ya barabara ya Lindi – Dar es Salaam katika eneo hilo ambalo
limekatika kutokana na mvua za El-Nino zilizonyesha zikiambatana na Kimbunga
Hidaya na kusababisha wananchi kukwamaa kwa siku kadhaa Mkoani Lindi.
![]() |
Waziri wa Ujenzi,
Innocent Bashungwa akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Zainab Telack pamoja na Mkuu
wa Wilaya ya Kilwa, Mohamed Nyundo na viongozi wengine wakikagua urejeshaji wa
miundombinu ya barabara ya Lindi –Dar es Salaam eneo la Somanga ambalo limeanza
kupitika Mkoani Lindi.
Bashungwa amezungumza
hayo Mei 08, 2024 Mkoani Lindi wakati akisimamia zoezi la urejeshaji wa
miundombinu ya barabara hiyo ambayo iliharibiwa mvua za El-Nino juzi Jumamosi ya
tarehe 04 Mei, 2024 zilizombatana na Kimbunga Hidaya.
“Kwa namnna
tulivyojipanga tuliahidi watanzania kuwa hadi kufikia Alhamisi barabara hii
tutakuwa tumerudisha mawasiliano na tayari kipande cha Somanga kilichokuwa kimekatika
kwa mita 200 tumeshakikamilisha na hivi sasa nguvu zote tunazielekeza katika
eneo la Songas na kuendelea katika maeneo mengine”, ameeleza Waziri Bashungwa.
Aidha, Bashungwa
ameeleza changamoto zinazowakabili wataalam ambao wanaendelea kurejesha mawasiliano
katika barabara hiyo ni upatikanaji wa mawe ambayo yanafuatwa Kigamboni na
Boko-Magereza Mkoani Dar es Salaam, huku zoezi hilo likifanyika usiku na
mchana.
“Lakini kwa vile zoezi
hili tunalifanya usiku na mchana pamoja na changamoto hizi tumeweza kurudisha
mawasiliano eneo la Somanga na nguvu hiyohiyo tunaiamisha katika maeneo
mengine”, ameeleza Waziri Bashungwa.
Pamoja na hayo
ameipongeza timu ya wataalamu ikiongozwa na Mtendaji Mkuu wa TANROADS,
Makandarasi na wasaidizi wake pamoja viongozi wa Wizara na Mkoa.
Naye, Mkuu wa Mkoa wa
Lindi, Zainab Telack amepongeza timu ya wataalam na Makandarasi kwa kufungua
eneo cha Somanga ambapo amesema ana imani na eneo la Songas napo mawasiliano
yataweza kurejea usiku wa leo Mei 08, 2024.
Kwa upande wake Mwenyekiti
wa Kijiji cha Somanga kusini, Mustafa Omari Mkunga ameishukuru Serikali kwa
kazi kubwa katika eneo la Somanga ambalo lililkuwa korofi na sasa limeweza
kupitika.


.jpg)

No comments:
Post a Comment