KATIBU MKUU WIZARA YA UTAMADUNI, AWATAKA VIJANA KUJITUMA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday 1 May 2024

KATIBU MKUU WIZARA YA UTAMADUNI, AWATAKA VIJANA KUJITUMA

Wapili Kulia ni Katibu Mkuu wizara ya Utamaduni , Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa katika picha ya Pamoja na Baba Halisi, Mama Halisi na wakwanza kulia ni Ofisa utamaduni kutoka Basata.

Wapili Kulia ni Katibu Mkuu wizara ya Utamaduni , Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa katika picha ya Pamoja na Baba Halisi, Mama Halisi na wakwanza kulia ni Ofisa utamaduni kutoka Basata.

Na Dunstan Mhilu

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa amewataka vijana nchini kote kujituma na kujikita zaidi katika uzalishaji mali.

Rai hiyo imetolewa jana wakati wa hafla ya uzinduzi wa Albam ya ‘Bila Chanzo Halisi hautoboi iliyoandaliwa na bendi ya kwaya ya Kanisa Halisi la MUNGU BABA lililopo Namanga Tegeta Dar es Salaam na uzinduzi wake kufanyika katika ukumbi wa Mlimani City mkoani Dar es Salaam.

“Wakati nikimsikiliza Baba Halisi, Kiongozi wa Kanisa hili nilikoshwa na maneno au nguzo kuu tatu za Kanisa hili, ambazo ni Utawala wa Amani, Upendo usiyobagua, na Ibada ni uzalishaji, yote ni maneno mazuri na yenye busara lakini Baba Halisi alienda mbali zaidi akisema kwamba hawataki watu waje Kanisani na kuzurura na badala yake wakazalishe kisha wamletee matunda aliyeumba” alisema Msigwa

Naye Msigwa akichagiza maneno ya Baba Halisi aliwataka vijana kufanya kazi kwa bidi na kujiepusha na matendo maovu na vitendo vya kiuharifu na kuwahakikishia vijana na Kanisa kwa ujumla kwamba serikali ipo karibu na Kanisa na vijana kwa ujumla na hivyo wasisite kubisha hodi serikalini.

Aidha amempongeza Baba Halisi, Mama Halisi, watenda kazi wote na uzao Halisi wa Kanisa hilo kwa mshikamano na upendo waliokuwa nao kama kanisa na kuwataka kuepukana na migogoro isiyokuwa na tija kwa kanisa na Taifa.

Kwa upande wake Baba Haalisi Kiongozi Mkuu wa Kanisa hilo alisema kwamba Kanisa hilo halijihusishi na siasa na badala yake huwaombea wanasiasa ili wawaongoze watanzania kwa hekima na amani kwakuwa ni wajibu wao kufanya hivyo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jana kiongozi wa kanisa Kituo cha Arusha, Amani Halisi alisema katika kanisa hilo wamekuwa wakifundisha amani kwa wote, ibada, upendo uliopitiliza, kufanya kazi na jamii inayowazunguka.

“Tuko hapa ili watanzania wajue kuwa kanisa Halisi lipo kwaajili yao”Aidha alisema mapokeo ya uzinduzi wa Albamu hiyo yamekuwa ni makubwa tofauti na awamu ya kwanza kwani takribani mataifa 7 yameshiriki na kusikilizwa na mataifa 130 Duniani.

“Mapokeo ni makubwa sana kwasababu leo tupo nje ya kanisa ambapo mataifa takribani 7 yameshiriki na tunasikilizwa na mataifa 130 Duniani, ndani ya makanisa ya Tanzania tuna makanisa 360”

Kuhusu Mchango wa Serikali, Amani alisema wameendelea kushirikiana nao bega kwa bega ambapo inapelekea Wana Halisi kwa ujumla kuendelea kuwafanyia maombi viongozi wote wa serikali.

“Mchango wa serikali inatupenda maana tunafanya kazi na serikali katika majira ya nyuma wenzetu waliopita hawakufanya kazi na serikali mfano Musa hakufanya na farao n.k, ila sisi kanisa Halisi tunafanya kazi na serikali na ndiyo maana Kila siku tunafanya maombi maalumu kwaajili ya serikali yetu”

Naye mtekeleza sauti lango Moja la mafanikio, kutoka kanisa la Halisi Mkoa wa Tanga aliwataka Wana Halisi waendelee kumuabudu muumbaji kwani ndiyo kusudi la aliyewaumba.

No comments:

Post a Comment