MENEJA TARURA, ATOA UFAFANUZI UBOVU WA BARABRA YA MTAA WA LINDI INAYOUNGANISHA MACHINGA COMPLEX - THE HABARII

THE HABARII

HABARI | MATUKIO | MICHEZO.


ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday, 1 May 2024

MENEJA TARURA, ATOA UFAFANUZI UBOVU WA BARABRA YA MTAA WA LINDI INAYOUNGANISHA MACHINGA COMPLEX

 

Meneja wa Tarura Mkoa wa Dar es Salaam, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu masuala ya miundombunu ya barabara mkoni Dar es Salaam.

Na Dunstan Mhilu

MENEJA Wa Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA), Mhandisi Geofrey Mkinga ametolea ufafanuzi wa ubovu wa barabra ya mtaa wa Lindi inayounganisha Machinga Complex, Mtaa wa Rahaleo na Gerezani kuhusiana na ubovu wa kipande hicho kidogo kuwa kibovu kwa kipindi kirefu bila kukarabatiwa.


Akizungumza na mwandishi wa habari, Mhandisi Mkinga alisema ni kweli kipande hicho ni korofi lakini zipo sababu ambazo Tarura mkoa na halmashauri ya wilaya ya Ilala haikukikarabati.


“Nikweli ndugu Mwandishi kazi yetu Tarura kama ijulikanavyo ni kuzijenga na kuzikarabati Barabara zote zilizopo chini ya Tarura lakini kwa bahati nzuri Dar es Salaam tuna miradi mingi ya Barabara ambapo tumegawana majukumu, Mathalani hiki kipande unachozungumzia kitakarabatiwa na ndugu zetu wa Mradi wa Mabasi yaendayo haraka DART na kipo katika mpango kazi wao

Ndiyo maana sisi hatujakikarabati na bajeti yake ipo na kwakuwa bado wapo katika utekelezaji wa mradi huo kitatengenezwa tu ni shida ya muda mfupi, hata hivyo jitihada za kumpata Mkurugenzi wa DART hakuzaa matunda baada ya simu yake kuita bila kupokelewa lakini gazeti hili linaendelea kufuatilia suala hilo ili lipatiwe ufumbuzi.


Kipande hicho ni sumbufu na kero kwa abiria wanaotumia njia hiyo kwa miguu na wanaotumia usafiri wakutoka Buza na Yombo Kilalakala ambapo safari zakutoka katika makazi yao huishia katika eneo hilo ambalo limekithiri madimbwi makubwa yanayosababisha hitilafu kwa magari husika.


Wakati huohuo, akizungumzia kuhusu maagizo na maelekzo ya Mtendaji Mkuu wa Tarura , Mhandisi Victor Seff kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila na Meneja wa Tarura mkoa wa Dar es Salaama aliyoyatoa miezi 3 iliyopita wakati wakikagua maeneo yaliyoathirika na Mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam.


Mhandisi Victor Seff aliaagiza kukarabatiwa haraka madaraja ya Tanganyika, Mbopo, Msumi na Goba Majengo pamoja na barabara zote zilizoharibika kutokana na mvua kubwa iliyonyesha mkoani humo na zinazoendelea kunyesha.

 

Mhandisi Mkinga alisema kwamba maagizo hayo yalitekelezwa mara moja na mwandishi wa gazeti hili alitembelea maeneo yote nakujionea ufanisi mkubwa uliofanywa na Tarura chini ya usimamizi mahiri wa Mhandisi Mkinga na wasaidizi wake.

 

“Tulifanya hivyo kama tulivyoelekezwa na ilikuwa kazi ya usiku na mchana ili kurejesha mawasiliano katika maeneo yote tajwa na hata sasa nikueleze Mwandishi hatulali kutokana na mvua inayonyesha haijalishi bajeti tulikuwa nayo ikoje lakini lengo ni mawasiliano yapatikane na Dar es Salaam ni Barabara na siyo vinginevyo ahsante” alisema Mhandisi Mkinga

 

Mhandisi Seff ametoa maagizo hayo mara baada ya kufanya ukaguzi kwenye madaraja yaliyosombwa na mvua kubwa iliyonyesha Januari20, 2024 na kujionea uharibufu uliotokea.

 

Mhandisi Seff aliwataka Tarura kufanya kazi usiku na mchana ili kurudisha mawasiliano ya miundombinu ya barabara zote na madaraja yaliyoharibika ili kuwezesha shughuli za kiuchumi na kijamii kuendelea kama awali na kufanya ukaguzi wa maeneo yaliyoathirika na mvua likiwemo daraja la Tanganyika lililosombwa na maji pamoja na maingilio ya barabara ya Salasala-Benako yenye urefu wa Km. 4.6 yaliyoharibika vibaya.

No comments:

Post a Comment