Baadhi ya Wanafunzi wa chuo hicho wakichangia damu. |
Na Dunstan Mhilu
MPANGO wa Taifa wa Damu Salama (NBTS) umewahamiza watanzania kujitolea kuchangia damu ili kutatua changamoto ya upatikanaji wad amu nchini.
Mwito ama wito huo umetolewa na Meneja wa NBTS Kanda ya Mashariki, Dk. Pendael Sifuel, wakati wa uchangiaji damu uliotekelezwa na Chuo cha Afya cha Excellent chenye makao yake makuu Dar es Salaam.
“Kimsingi ipo haja jamii kuchangia damu kwa manufaa yetu wenyewe kwani pamoja na jitihada mbalimbali zinazofanywa na NTBS na serikali kwa ujumla upo mwitikio mdogo sana wa uchangiaji damu na hivyo tunawahimiza wananchi kuchangia damu kwa akiba yao wenyewe” amesema Sifuel.
Dk. Sifuel alisema kwa mwaka Mpango wa Taifa wa Damu Salama unahitaji walau chupa 600,000 za damu ili kufikia malengo. Pamoja na idadi kubwa ya Watanzania wapatao 61.7 milioni bado kuna mwitiko mdogo wad amu.
“Tanzania kwa idadi ya watu wake siyo wakuwa na uhaba wa damu, mathalani mkoa wa Dar es Salaam pekee una watu takribani 5,282,728 ambapo wangelichangia kwa asilimia moja tu ni sawa na watu 50,000 wakijitokeza hao hata kwa chupa moja moja je tuna chupa ngapi? Hamsini je enda wakatoka 600, 000 tu wa Dar es Salaam nje ya watu milioni tano? Jumlisha na mikoa yote Bara na Visiwani tungelikaa hata miaka kadhaa hatuchangii damu,” amesema Dk, Sifuel.
Kwa upande wake mkuu wa chuo cha Excellent Dk. Johanes Joas amesema wao kama wadau wakuu wa afya na mtaji wa binadamu huchangia damu kila mwaka na hii ni mara ya saba na wanataka kuchangia mara kwa mwaka.
“Mwandishi kama ujuavyo sisi tunabidhaisha afya ya binadamu kuanzia chuoni hadi sokoni huku tukisisitiza afya njema, kama ndivyo hatunabudi kuwa mstari wa mbele kuhakikisha damu ya kutosha inapatikana katika benki yad amu popote pale chuo chetu kilipo ndiyo maana wanafunzi wetu wamejitolea kwa moyo mkunjufu pasipo kulazimishwa,” amesema Dk, Joas.
Jumla ya chupa 146 zilipatikana katika kampeni ya uchangiaji damu kwa hiari uliofanyika chuoni hapo eneo la Boko Dar es Salaam makao makuu ya chuo hicho ambapo kina wanafunzi 900 na na 500 katika Kampasi za Kibaha na Mwanza.
Hata hivyo mkuu huyo wa chuo amesema huenda wangelichangia chupa nyingi zaidi kama muda ungelikuwa unatosha nakuahidi kuendelea kuchangia damu.
No comments:
Post a Comment