NAIBU WAZIRI WA USHIRIKIANO WA MAENDELEO WA SWEDEN AZURU NCHINI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Friday 22 March 2024

NAIBU WAZIRI WA USHIRIKIANO WA MAENDELEO WA SWEDEN AZURU NCHINI

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaib Mussa akimlaki Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Maendeleo wa Sweden, Mhe. Diana Janse mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa jijini Dodoma.

NAIBU Waziri wa Ushirikiano wa Maendeleo wa Sweden, Mhe. Diana Janse amewasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili kuanzia tarehe 21 – 22 Machi, 2023 na kupokelewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaib Mussa jijini Dodoma.

Lengo la ziara hiyo ni kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia na kiuchumi uliopo kati ya Tanzania na Sweden. Pia kupitia ziara hiyo Serikali ya Sweden inatarajiwa kueleza dhamira ya kuongeza muda wa Mpango wa Maendeleo unaotarajiwa kafikia ukomo mwaka huu 2024.

 

Baada ya kuwasili Mhe. Janse amefanya mazungumzo na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Deogratius Ndejembi (Mb.) ambapo katika mazungumzo yao wamejadili juu ya kuimarisha ushirikiano katika sekta za viwanda, biashara, uwekezaji na ujenzi wa miundombinu hususan uendelezaji wa mradi wa mabasi yaendayo kasi (Bus Rapid Transit Project).

 

Viongozi wengine aliofanya nao mazungumzo jijini Dododma ni pamoja na, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo (Mb.) na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb.)

 

Vilevile, Mhe. Janse anatarajia kufanya mazungumzo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk tarehe 22 Machi 2022 katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.

 

Tanzania na Sweden zilianzisha ushirikiano tangu mwaka 1960 ambapo nchi hizo zimekuwa zikishirikiana katika utekelezaji wa miradi mbalimbali katika sekta za nishati, tafiti, elimu, usimamizi wa mazingira, uchangiaji wa bajeti ya Serikali, biashara, viwanda, uwekezaji na miundombinu.

No comments:

Post a Comment