![]() |
| Muonekano wa barabara ya Mtwara-Mingoyo-Masasi katika eneo la Maili Mbili ambapo Daraja lilosombwa na maji kutokana na Mvua za Elnino zinazoendelea kunyesha nchini. |
![]() |
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa akizungumza na Wananchi wa Masasi Mara baada ya kukagua na kujionea daraja lililobomoka eneo la Maili Mbili katika barabara ya Mtwara-Mingoyo-Masasi mkoani Mtwara, tarehe 04 Machi 2024.
WAZIRI wa Ujenzi,
Innocent Bashungwa ameelekeza Wakala wa Barabara (TANROADS) kuhakikisha
wanarejesha mawasiliano ya barabara iliyokatika eneo la Maili Mbili katika
barabara ya Mtwara-Mingoyo-Masasi ndani ya masaa matatu mara baada ya Daraja
kusombwa na maji katka eneo hilo.
Bashungwa ametoa agizo
hilo tarehe 04 Machi, 2024 Wilayani Masasi akiwa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais
- TAMISEMI, Deo Ndejembi, alipofika hapo kujionea adha ya watumiaji wa barabara
hiyo waliokwama tangu majira ya asubuhi kutokana na kukatika kwa miundombinu
hiyo iliyosababishwa na mvua kubwa
zilizonyesha usiku wa jana.
“Nitoe pole kwa
wananchi ambao mmepata changamoto kutokana na kukatika kwa mawasiliano ya
barabara inayotoka mkoa wa Ruvuma kuelekea mkoa wa Mtwara na Lindi, Natoa saa
tatu kwa TANROADS kuhakikisha inakamilisha kujenga barabara ya mbadala ili
magari na wananchi waanze kupita", amesisitiza Bashungwa.
Bashungwa ameeleza
kuwa tayari Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshatoa fedha za kumtafuta
Mkandarasi atakayeijenga upya barabara hiyo ya Mtwara-Mingoyo-Masasi (km 200)
kwa kiwango cha lami kwa kuwa barabara hiyo imekwisha muda wake na imechakaa.
“Wizara ya Ujenzi
tumeshapokea maelekezo ya Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan hadi
kufikia Mwezi wa Sita Mkandarasi awe ameshapatikana na kuanza kazi ya kuijenga
upya barabara hii”, amefafanua Bashungwa.
Naye, Naibu Waziri
Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Deo Ndejembi ameeleza kuwa Rais, Dkt. Samia Suluhu
Hassan ameshatoa kiasi cha Shilingi Bilioni 30 kwa ajili ya dharura za
matengenezo ya barabara nchi nzima kupitia Wakala wa Barabara Vijijini na
Mijini (TARURA) na hivyo wamejipanga vyema kutatua changamoto zozote za
mawasiliano ya barabara pindi zinapotokea.
Kwa upande wake Mbunge
wa Masasi, Geofrey Mwambe, ameishukuru Serikali na timu nzima ya watalaam wa
TANROADS kwa kuchukua hatua za haraka za kuhakikisha wanaanza kazi ya kurejesha
mawasiliano ya barabara hiyo na miundombinu mingine ambayo imeathiriwa na mvua
katika Wilaya ya Masasi.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi
.jpeg)
.jpeg)

No comments:
Post a Comment