MKUU WA KITENGO CHA MAWASILIANO WIZARA YA FEDHA AKAGUA MIUNDOMBINU YA HABARI MTUMBA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday, 25 January 2024

MKUU WA KITENGO CHA MAWASILIANO WIZARA YA FEDHA AKAGUA MIUNDOMBINU YA HABARI MTUMBA

 

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, Wizara ya Fedha, Bw. Benny Mwaipaja (katikati) na Mtaalamu wa Ujenzi wa Studio za Habari kutoka Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Bw. Karim Chitenda (kulia) wakisikiliza maelezo ya, Mhandisi wa Jengo jipya la Wizara ya Fedha Mtumba, David Shunu, wakati Mkuu huyo wa Kitengo cha Mawasiliano alipotembelea na kukagua miundombinu ya Mawasiliano katika jengo jipya la Wizara ya Fedha, Mtumba, jijini Dodoma.

Mtaalamu wa Ujenzi wa Studio za Habari kutoka Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Bw. Karim Chitenda (katikati) akieleza kuhusu mazingira ya Studio za Habari kwa Mhandisi wa Jengo jipya la Wizara ya Fedha Mtumba, David Shunu wakati Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, Wizara ya Fedha, Bw. Benny Mwaipaja (kushoto) alipotembelea na kukagua miundombinu ya Mawasiliano katika jengo hilo, jijini Dodoma.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, Wizara ya Fedha, Bw. Benny Mwaipaja akizungumza kuhusu miundondombinu ya Mawasiliano na Mhandisi wa Jengo jipya la Wizara ya Fedha Mtumba, David Shunu, alipotembelea na kukagua miundombinu ya Mawasiliano katika jengo hilo, jijini Dodoma.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, Wizara ya Fedha, Bw. Benny Mwaipaja akizungumza na Wahandisi wa Jengo jipya la Wizara ya Fedha Mtumba pamoja na Mtaalamu wa Ujenzi wa Studio za Habari kutoka Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Bw. Karim Chitenda, alipotembelea na kukagua miundombinu ya Mawasiliano katika jengo hilo, jijini Dodoma.

No comments:

Post a Comment