![]() |
Hayo
yameelezwa na Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa leo tarehe 25 Januari 2025
wakati akizingumza na wananchi wa Lituhi mara baada ya kukagua barabara hiyo
ambayo ipo katika hatua za kusainiwa mkataba.
Hayo
yameelezwa na Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa leo tarehe 25 Januari 2025
wakati akizingumza na wananchi wa Lituhi mara baada ya kukagua barabara hiyo
ambayo ipo katika hatua za kusainiwa mkataba.
Bashungwa
amesema ujenzi wa barabara hiyo utawezesha meli za mizigo hasa makaa ya mawe
ziweze kupakia kupitia Bandari ya Ndumbi kwenda sehemu mbalimbali za nchi
yetu na nchi jirani za Malawi na
Msumbiji.
Ameongeza
kuwa barabara hiyo inaunganisha Mkoa wa Ruvuma na Njombe kupitia Daraja la
Ruhuhu ambayo itafungua fursa za maendeleo na biashara.
Bashungwa
ameagiza Wakala wa Barabara (TANROADS), kumsimamia Mkandarasi atakayepatikana
kwa karibu ili mradi huo ukamilike kwa viwango.
Kwa
upande wake, Mbunge wa Nyasa, Mhe. Eng. Stella Manyanya, amemuomba Waziri huyo
kuwajengea angalau madaraja maeneo korofi hasa katika vipindi vya mvua kwani
imekuwa Kero kwa wananchi wake.
Eng.
Manyanya ameomba kipande cha barabara kutoka Mbambabay hadi Chiwimbi (km 45)
ipewe kipaumbele kwa kuwa ni barabara muhimu na ya Ulinzi ambayo inaunganisha
nchi ya Tanzania na Msumbiji, hivyo anaomba ipewe kipaumbele.
“Barabara
ya kutoka Nyoni- Matomoni haimo kwenye ilani ila tulikuwa tunaomba ifanyiwe
upembuzi yakinifu kwa sababu ni barabara ya uchumi, Kahama yote inatoka huko”
ameongeza Eng. Manyanya.


No comments:
Post a Comment