BARABARA YA KIDATO-IFAKARA KUKAMILIKA MACHI 2024 - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday, 25 January 2024

BARABARA YA KIDATO-IFAKARA KUKAMILIKA MACHI 2024

Naibu Waziri wa Ujenzi Eng.  Godfrey Kasekenya akikagua Daraja la Ruaha na barabara ya Kidato-ifakara ambayo ujenzi wake unaendelea mkoani Morogoro

Naibu Waziri wa Ujenzi Eng.  Godfrey Kasekenya akikagua daraja la Ruaha na barabara ya Kidato-ifakara ambayo ujenzi wake unaendelea mkoani Morogoro


Naibu Waziri wa Ujenzi Eng.  Godfrey Kasekenya akikagua daraja la Ruaha na barabara ya Kidato-ifakara ambayo ujenzi wake unaendelea mkoani Morogoro.

NAIBU Waziri wa Ujenzi Mhandisi Godfrey Kasekenya amesema kufikia Machi 2024 Serikali imejipanga kukamilisha ujenzi wa Barabara ya Kidato-Ifakara yenye urefu wa KM 66.9 pamoja na daraja la Ruaha lenye mita 133.

Kasekenya ameyasema hayo baada ya kukagua eneo hilo la ujenzi Wilayani Ifakara  mkoani Morogoro nakueleza kuwa barabara hiyo imekuwa changamoto kubwa kwa watumiaji kwa muda mrefu hivyo serikali imeahidi kuimaliza, lengo kubwa ikiwa ni kurahisisha usafiri na usafirishaji wa bidhaa ili kukuza uchumi wa wananchi na taifa kwa ujumla kwa kuwa eneo hilo lina uzalishaji mkubwa.

No comments:

Post a Comment