Na, Brown Jonas – WUSM,
Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.
Dkt. Damas Ndumbaro amekabidhi mashine mbili za kukatia nyasi katika uwanja wa
mpira wa miguu wa CCM Majimaji kwa uongozi wa chama hicho Mkoa wa Ruvuma.
Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amekabidhi mashine hizo leo Desemba 21, 2023 mjini
Songea ikiwa ni utekelezaji wa azma ya Serikali kufanya maboresho katika
viwanja mbalimbali nchini.
Amesema kuwa kukarabatiwa kwa uwanja huo kutawezesha vilabu mbalimbali
nchini kuutumia uwanja huo kwa mechi za ligi kuu jambo ambalo litaongeza hamasa
ya soka mkoani humo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma Ndg. Odo Mwisho ameishukuru
Serikali ya Awamu ya Sita kwa jitihada mbalimbali inazofanya kuboresha sekta ya
michezo nchini hususani mkoa wa Ruvuma ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya
Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2020-2025.
Makabidhiano ya mashine hizo zenye thamani ya Shilingi Milioni saba
yameshuhudiwa na Mkuu wa Wilaya ya Songea Mjini Bw. William Kapenjama na
viongozi wengine wa chama na serikali ambapo pia Mbunge wa Jimbo hilo na Waziri
wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amemleta mtaalam
atakayetoa mafunzo kwa wasimamizi wa uwanja kuhusu matumizi ya mashine
hizo uwanjani hapo.

No comments:
Post a Comment