Na Mwandishi Wetu
SERIKALI imesema
Tanzania ina mazingira mazuri ya uzalishaji wa mazao ya nyuki yenye kiwango cha
juu cha ubora kutokana na uwepo wa misitu yenye mimea inayotoa chakula kwa
nyuki huku sekta hiyo ikichangia ajira zaidi ya ajira ya watu milioni mbili na
kukadiliwa kuwa na uwezo wa uzalishaji wa asali tani 138,000 kwa mwaka.
Akizungumza
katika uzinduzi wa kitaifa wa ugawaji wa mizinga 500 iliyotolewa na benki ya
NMB wilayani Gairo mkoani hapa, Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dk
Hassan Abbas amesema uzalishaji watani 138,000 za asali ya nyuki kwa mwaka ni
kiwango kidogo ikilinganishwa na fursa zilizopo na tathmini iliyofanywa na
wizara hiyo inaonesha kuwa asilimia 90 ya wafugaji nyuki nchini wanatumia
mizinga ya jadi.
Dk Abbas amesema
mizinga hiyo ya jadi inachangia uharibifu wa misitu kwani utengenezaji wake
unahusisha ukataji wa miti hivyo wadau na serikali wanajukumu la kuendeleza
sekta hiyo kwa kuandaa mazingira mazuri ya upatikanaji wa mizinga ya kisasa
ambayo italeta tija na kulinda misitu.
“Mizinga ya jadi
inazalisha kiwango kidogo cha asali lakini asali ya Tanzania inakubalika kwenye
masoko mbalimbali nje ya nchi sekta za misitu na ufugaji nyuki zinachangia
wastani wa asilimia 3.5 ya pato ghafi la taifa ukilinganisha na fursa za rasilimali
za misitu na nyuki zilizopo na niwaombe wenzetu wa NMB kuongeza mizinga ya
kisasa ifikie 600 wakati serikali ikiandaa na kutekeleza mikakati ya ujenzi wa
viwanda ambavyo kwa sasa vipo sana vya kuchakata na kufungasha mazao ya
nyuki.”amesema Dk Abbas.
Juhudi hizi pia
ni sehemu ya maandalizi yetu kuelekea Mkutano Mkuu wa Wafugaji Nyuki Duniani
utakaofanyika Tanzania mwaka 2027, ambao utawahusisha waataalum
wakimataifa zaidi ya 4000.
Kwakweli Benki ya
NMB mnastahili pongezi kubwa sana kwa kuzindua Programu Endelevu ya Ugawaji
Mizinga ya Nyuki 500 kwa vikundi 17 vyenye wafugaji zaidi ya 300, katika mikoa
ya Morogoro, Tabora na Njombe, mkishirikiana na Mamlaka ya Uhifadhi wa Misitu
Tanzania (TFS).
Afisa mkuu wa
wateja wakubwa na serikali benki ya NMB, Alfred Shao amesema benki hiyo
imewezesha kutengeneza mizinga 500 ya kisasa kwa ajili ya kuwagawia wafugaji
nyuki katika mikoa ya Morogoro, Tabora na Njombe.
Shao amesema
licha ya kutoa mizinga hiyo, benki hiyo imetenga sh41milioni kwa ajili ya kuwezesha
mafunzo kwa wanufaika wa mizinga hiyo katika mradi wa kusapoti ufugaji wa
nyuki.
“Nyuki ili
wazaliane ni lazima misitu ilindwe na moja ya sababu ya NMB kutoa mizinga hii
500 ni juhudi za kulinda misitu yetu ikienda sambamba na upandaji miti ambapo mpaka
sasa miti 750,000 tayari imepandwa nchini kwa kushirikiana na TFS na wananchi
wanapata mazao ya misitu kwa kutunza mazingira.”amesema Shao.
Shao amesema
benki ya NMB kupitia NMB Foundation imetoa mizinga 500 ya kisasa kwa mikoa
mitatu ambapo mkoa wa Morogoro umepata mizinga 200, Tabora 200 na Njombe 100
kwa vikundi 17 vya ufugaji nyuki na vikundi hivyo vitapatiwa elimu ya ufugaji
nyuki wa kisasa, elimu ya kifedha na elimu ya uvunaji wa asali ili asali
itayovunwa iwe ya ubora wa kiwango cha juu na kuuzwa nje ya nchi.
Serikali ya Rais
Samia imeweka mkazo mkubwa katika sekta ya asali na nyuki, ambako tayari kuna
Watanzania takribani milioni mbili wamejiari huko, na tunatambua hii ni sekta
ya kimkakati ambayo ikitiliwa mkazo, itawakwamua wengi, vijana tuipe mkazo
sekta hiyo ambayo ni itakuwa ya kijanja zaidi huko tuendako, yenye ‘maokoto’ ya
kutosha,aliongeza Dk. Abbas.
“Usisubiri NMB
waje, anza leo wakukute pazuri. Sekta hii inachangia Pato la Taifa kwa asilimia
3.5, pia mazao ya misitu na asali yanachangia asilimia 5.9 ya fedha za kigeni,
huasusani Dola za Kimarekani, sio sekta yenye eneo dogo, bali ina mawanda
mapana, vijana wasidharau sekta zenye kuingiza pesa kama hii, ambayo Serikali
hatulali kwa kuchakata mipango mikubwa juu yake.
“Tumeanza ujenzi
wa viwanda saba vya kuchakata na kufungasha asali, ili kukuza uchumi ambako
Serikali imewekeza zaidi ya Sh. Bilioni 2 katika mikoa ya Tabora, Katavi,
Geita, na Kigoma, NMB mtapoenda huko mtawakuta wafugaji. Mradi mwingine ni wa
Sh. Bilioni 27 wa kujenga madarasa na mabweni ya Chuo cha Ufugaji Nyuki Tabora,
NMB tunawaomba mje kuona uwekezaji wetu,” alibainisha.
Dk. Abbas
aliongeza ya kwamba, Rais Samia hivi karibuni amefanya uamuzi mgumu wa
kimkakati, kwa kuiingiza sekta ya asali na nyuki katika Programu ya Kujenga
Kesho Iliyo Bora kwa Vijana na Wanawake nchini (BBT), hivyo akaziomba Sekta za
Fedha na Sekta Binafsi, zifuate nyayo za NMB kwa kuisapoti Serikali katika
kuipa thamani zaidi Kampeni ya Achia Shoka, Kamata Mzinga.
“Tutawaalika wadau
tutapokamilisha kampeni hiyo waone jinsi ya kusaidiana na Serikali, ili kutanua
sekta hii kuelekea Mkutano Mkuu wa Wafugaji Nyuki Duniani hapo mwaka 2027,
utakaowaleta nchini zaidi ya washiriki 4,000 kutoka mataifa mbalimbali duniani.
Mkutano huo ni uthibitisho wa Jumuiya ya Kimataifa kuridhishwa na hatua
iliyopigwa na Serikali ya Rais Samia,” alisisitiza.
Naye Mkuu wa
wilaya ya Gairo, Jabir Makame amesema programu ya boresha mazingira na uchumi
kupitia ugawaji wa mizinga kitaifa kufanyika wilaya ya Gairo na wataendelea
kuwapa hamasa jamii ya wilaya hiyo kuendelea kuhifadhi na kutunza mazingira.
Kamishna wa
Uhifadi Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) TFS, Profesa Dos Santos
Silayo amesema benki ya NMB imekuwa na ushirikiano nao katika utunzaji
mazingira na upandaji miti tangu mwaka 2022 na sekta ya ufugaji nyuki
inaonekana kama ni kazi ya wazee na kuwekeza nguvu utawafanya riba nyingine
kuona tija katika sekta hiyo.


.jpg)
.jpg)
.jpg)

No comments:
Post a Comment