TTCL YAWEZESHA MAWASILIANO YA INTANETI MKUTANO WA PAPU, JIJINI ARUSHA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Saturday, 2 September 2023

TTCL YAWEZESHA MAWASILIANO YA INTANETI MKUTANO WA PAPU, JIJINI ARUSHA

Waziri wa Mawasiliano nchini Afrika Kusini Bw. MONDLI GUNGUBELE akipeana mkono na Meneja wa TTCL Mkoa wa Arusha Bw. FREDRICK MLOKA wakati alipotembelea Banda la TTCL kwenye maonesho yaliyoandaliwa na Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wakati wa Kikao cha 41 cha Baraza la Umoja wa Posta Afrika kinachofanyika jijini Arusha.


Naibu Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Mhandisi Kundo Mathew akimwelezea Waziri wa Posta na Mawasiliano wa Liberia Bw. WORLEA SAYWAH DUWAH huduma ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano inayosimamiwa na kuendeshwa na Shirika la Mawasiliano Tanzania -TTCL

Baadhi ya wajumbe wa Mkutano wa 41wa Baraza la Umoja wa Posta Afrika (PAPU) wakitembelea Banda la Shirika la Mawasiliano Tanzania-TTCL kwenye maonesho yaliyoandaliwa na Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na kuoneshwa miundombinu ya kimkakati ya mawasiliano inayosimamiwa na shirika hilo.


Baadhi ya wajumbe na viongozi anuai wakipata maelezo juu ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na TTCL walipotembelea banda la shirika hilo kwenye maonesho yanayoendelea nje ya Mkutano wa 41wa Baraza la Umoja wa Posta Afrika (PAPU).

Baadhi ya viongozi na wajumbe wa Mkutano wa 41wa Baraza la Umoja wa Posta Afrika (PAPU) wakisaini kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea Banda la Shirika la Mawasiliano Tanzania-TTCL kwenye maonesho yaliyoandaliwa na Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na kuoneshwa miundombinu ya kimkakati ya mawasiliano inayosimamiwa na shirika hilo.

Baadhi ya wajumbe wa Mkutano wa 41wa Baraza la Umoja wa Posta Afrika (PAPU) wakitembelea Banda la Shirika la Mawasiliano Tanzania-TTCL kwenye maonesho yaliyoandaliwa na Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na kuoneshwa miundombinu ya kimkakati ya mawasiliano inayosimamiwa na shirika hilo.

Na Mwandishi Wetu, Arusha

SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania-TTCL limewezesha huduma za mawasiliano ya intaneti kwa wajumbe wanaoshiriki Kikao cha 41 cha Baraza la Umoja wa Posta Afrika kinachofanyika jijini Arusha, ikiwa ni kuhakikisha mkutano huo unafanikiwa kwa mujibu wa malengo tarajiwa. Shirika la TTCL ni miongoni mwa Taasisi na Mashirika ya Umma yaliyochini ya Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari yanayoshiriki pia maonesho yaliyoandaliwa na Wizara hiyo pembezoni mwa Kikao cha 41 cha Baraza la Umoja wa Posta Afrika kinachofanyika jijini Arusha. 

Akizungumza pembezoni mwa mkutano huo, Meneja wa Banda katika maonesho hayo yanayofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa (AICC), Bw. Laibu Leonard alisema TTCL katika kuchagiza maendeleo ya sekta ya mawasiliano pia imejenga miundombinu ya mawasiliano kupitia Mkongo wa Taifa kwenye Jengo jipya la Makao Mkuu ya Umoja wa Posta Afrika linalotarajiwa kuzinduliwa kesho jijini Arusha.

Akifafanua zaidi, Bw. Leonard alisema Shirika la TTCL inafuraha kushiriki katika maonesho hayo kwani imepata fursa ya kuendelea kuifungua nchi katika sekta ya utalii, hasa kwa kitendo cha kuwezesha washiriki katika eneo hilo kushuhudia matukio ya moja kwa moja yanayoendelea katika watalii wanaopanda na kushuka katika Mlima Kilimanjaro.

Bw. Leonard amesema kupitia maonesho hayo nchi 30 kati ya nchi wanachama 45 wa Umoja wa Posta Afrika (PAPU) zimenufaika na kasi ya mtandao iliyotolewa na TTCL na hivyo kuziwezesha kufanikisha matukio mbalimbali yanayojadiliwa kimaendeleo katika Kikao hicho.

Aidha ameongeza kuwa TTCLimebeba dhamana ya kuhakikisha washiriki wote wanapata mtandao wa uhakika na kasi ili dhamira ya kikao hicho ya kufanya shughuli za Posta kufanyika kidigitali iweze kuonekana inatekelezeka. 

"Shirika letu tunawaunganishia washiriki wote hapa Wireless ya bure yenye kasi ya 10G no mtandao wa uhakika na haukwamikwami na hapa pia tunaonesha Moja kwa moja matukio yanayoendelea katika mlima Kilimanjaro kwanzia mwanzo mpaka Uhuru Peak," amesema Laibu.

Ameongeza kuwa kupitia maonesho ya Banda la TTCL ni wazi watavutiwa na upo uwezekano kwa baadhi wakimaliza Mkutano wanaweza kwenda kutembelea mlima huo ili kujionea vivutio mbalimbali vinavyopatikana katika Hifadhi ya mlima Kilanjaro.

Aidha amesemaNa Kupitia Mkutano huu wa PAPU  Shirika (TTCL) limepata fursa ya kuonyesha huduma zake kwa wageni ambapo huduma hizo ni pamoja na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano (NICTBB) huduma za Data Center (NIDC) hivyo washiriki wameweza kupata uelewa wa namna miradi hii ya kimkakati inavyosamiwa na umuhimu wake kwa Wananchi.

Hata hivyo, amesisitiza kuwa kuwa maonesho hayo yanafanyika kuelekea Siku ya Uzinduzi wa Jengo la  Makao Makuu ya Umoja wa Posta Afrika (PAPU) utakaofanyika Septemba 2 Mwaka huu ambapo mpaka sasa TTCL wameshafikisha huduma ya Faiba katika Jengo hilo ili kuhakikisha shughuli zote za kiposta zinatekelezeka kidigitali. 

TTCL kama msimamizi na mwendeshaji wa miradi ya mawasiliano ya kimkakati linatekeleza majukumu yake ya kuhakikisha miundombinu ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano inajengwa nchini hadi nje ya mipaka ya Tanzania ili kuziwesha shughuli za Posta ndani na nje ya Afrika kufanyika vizuri.


No comments:

Post a Comment