MENEJIMENTI YA SEKTA YA UJENZI YAKAGUA JENGO LA WIZARA, MTUMBA JIJINI DODOMA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday 26 July 2023

MENEJIMENTI YA SEKTA YA UJENZI YAKAGUA JENGO LA WIZARA, MTUMBA JIJINI DODOMA

 

Sehemu ya menejimenti ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), wakikagua maendeleo ya ujenzi wa jengo jipya la Ofisi la Wizara hiyo, eneo la Mtumba, jijini Dodoma.

Sehemu ya menejimenti ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), wakitoka kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo jipya la Ofisi la Wizara hiyo, eneo la Mtumba, jijini Dodoma.

Muonekano wa hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi eneo la Mtumba, jijini Dodoma. Jengo hilo limefikia asilimia 68.

Msimamizi wa mradi wa jengo la Ofisi la Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kutoka Sekta ya Ujenzi, Eng. Paul Luhala, akiongoza menejimenti ya Sekta hiyo katika ukaguzi wa jengo  hilo ambalo limefikia asilimia 68, eneo la Mtumba, jijini Dodoma.

Mhandisi wa Mradi wa Jengo la Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kutoka Vikosi vya Ujenzi, Eng. Stanslaus Mkude, akitoa taarifa ya maendeleo ya ujenzi huo kwa Kaimu Katibu Mkuu ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Ujenzi wa Viwanja vya Ndege (Sekta ya Ujenzi) Qs. Mwanahamisi Kitogo, pamoja na Menejimenti ya Sekta hiyo wakati ilipokagua maendeleo ya ujenzi wa Ofisi ya Wizara hiyo eneo la Mtumba, jijini Dodoma.

No comments:

Post a Comment