BARABARA YA BUHIGWE - KASULU KM 35 KUKAMILIKA KWA LAMI OKTOBA MWAKA HUU - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday 31 July 2023

BARABARA YA BUHIGWE - KASULU KM 35 KUKAMILIKA KWA LAMI OKTOBA MWAKA HUU

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Mkoa wa Kigoma, Mhandisi Narcis Choma baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Barabara ya Chankere hadi Mwamgongo inayojengwa kwa kiwango cha zege, Mkoani Kigoma.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa akisisitiza jambo kwa Viongozi wa Wilaya ya Buhingwe, Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) na Mkandarasi wa Kampuni ya ZCCC mara baada kukagua barabara ya Kasulu-Buhigwe- Manyovu yenye urefu wa kilomita 56, Mkoani Kigoma.

Muonekano wa hatua iliyofikiwa ya mradi wa barabara ya Kasulu-Buhigwe- Manyovu yenye urefu wa kilomita 56 inayojengwa kwa kiwango cha lami, Mkoani Kigoma.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa akimsikiliza Mkandarasi wa kampuni ya Synohydro Corporation Limited inayojenga barabara ya Kanyani Junction hadi Mvungwe yenye urefu wa Kilomita 70.5, wakati Waziri huyo alipokagua barabara hiyo, Mkoani Kigoma.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Wakandarasi Kampuni ya Synohydro Corporation Limited mara baada ya kukaugau mradi wa ujenzi wa barabara ya Kanyani Junction hadi Mvungwe yenye urefu wa Kilomita 70.5inayojengwa na kampuni hiyo, Mkoani Kigoma.

 

No comments:

Post a Comment