Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dkt Amos Nungu akizungumza na Wahariri wa Vyombo vya Habari leo Jijini Dar es salaam, kuhusu Kongamano la Kitaifa la Nane la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH).
(PICHA NA JOHN BUKUKU)
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dkt Amos Nungu akimsililiza Mkurugenzi wa Menejimenti ya Maarifa (DKM), Mha. Samson J. Mwela wakati akifafanua mambo kadhaa kwa Wahariri wa Vyombo vya Habari leo Jijini Dar es salaam, kuhusu Kongamano la Kitaifa la Nane la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH).
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dkt Amos Nungu akimsililiza Mkuu wa Kitengo cha Habari, Uhusiano na Mawasiliano kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Bi. Slivia Lupembe wakati akifafanua jambo Katika kikao hicho.
Meneja wa machapisho na hifadhi hati , Dkt. Bunini Manyilizu akijibu baadhi ya maswali ya wahariri wa vyombo vya habari.
Na Immaculate Makilika - MAELEZO
SERIKALI imesema kuwa imejipanga kuhakikisha sayansi na teknolojia inatumika ili kuleta chachu katika maendeleo nchini.
Akizungumza na Wahariri wa Vyombo vya Habari Jijini Dar es salaam, kuhusu Kongamano la Kitaifa la Nane la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dkt. Amos Nungu amesema kuwa lengo la kongamano hilo ni kuwaleta pamoja wadau ambao ni Serikali, wabunifu, watafiti pamoja na wananchi, na kutoa fursa mbalimbali zitakazo wanufaisha wadau hao.
"Kupitia Kongamano hili tunatoa fursa kwa wadau wetu ya kukutana, kuhabarishana, kujifunza na kuendeleza shughuli zao,” alieleza Dkt. Nungu.
Aidha, Dkt. Nungu alisema kuwa Kongamano hilo litakalofanyika Juni 14 - 16, 2023, jijini Dar es salaam, ambapo litahudhuriwa na washiriki 500 kutoka ndani na nje ya nchi. Pia, kutakuwa na mada mbalimbali zinazolenga kuangalia mfumo wa sayansi pamoja na ubunifu na mchango wake katika uchumi.
Alitaja baadhi ya mada kuwa ni uchumi wa kijani, sayansi huria, ubunifu wa maendeleo ya watu na mchango wa maarifa asilia.
Naye, Mkuu wa Kitengo cha Habari, Uhusiano na Mawasiliano kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Bi. Slivia Lupembe alisema kuwa Serikali kupitia wizara yake imejipanga kuhakikisha sayansi na teknolojia inakuwa chachu ya maendeleo na ndio maana imeendelea kufadhili kazi mbalimbali za kibunifu sambamba na kurasimisha kazi zao ikiwa ni pamoja na kuwasajili ili kuwatambua rasmi.
No comments:
Post a Comment