WATENDAJI WA OFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR KUTEMBELEA MIRADI YA TASAF UTETE RUFIJI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday 30 May 2023

WATENDAJI WA OFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR KUTEMBELEA MIRADI YA TASAF UTETE RUFIJI

Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Ladislaus Mwamanga (katikati) akizungumza na Watendaji kutoka Ofisi ya Makamu wa pili wa Rais wa Wanzibar na watendajiwa TASAF kutoka visiwani humo, walipotembelea ofisi za TASAF Dar es Salaam wakiwa njiani kwenda Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji kwa ziara ya mafunzo Jumanne Mei 30, 2023.

Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usimamizi wa Miradi ya TASAF Mwajuma Mussa Ali, Kaimu Sheha wa Kizimkazi Kasim Fadhili Ramadhan, Mratibu wa TASAF Unguja Makame Ali Haji na Meneja wa Uratibu na Itifaki wa TASAF, Tunu Munthali.

Bw Mwamanga aliwapongeza watendaji hao kwa kazi nzuri na kuwataka kuhamasisha wanufaika waliofanikiwa kujikwamua kuichumi kukubali kuondolewa kwenye Mpango wa Kunusuru Kaya za Walengwa kwa hiari yao ili kuwapa nafasi wengine kunufaika. Watendaji hao wako katika ziara ya siku mbili katika Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji kujifunza usimamizi wa miradi ya TASAF

Kaimu Sheha wa Kizimkazi Kasim Fadhili Ramadhan Katika Ofisi za TASAF wakati watendaji wa taasisi hiyo walipozungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Ladislaus Mwamanga kulia, Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usimamizi wa Miradi ya TASAF Mwajuma Mussa Ali.

Donald Mkisi Mkurugenzi wa Utawala na Fedha TASAF akishishiriki Katika kikao hicho.

John Stephen Mkurugenzi wa Huduma za Jamii TASAF na Khalid  Bakari Hamran Mratibu Mkuu wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar SMZ Kwa upande wa Tanzania Bara Dodoma.

Picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladslaus Mwamanga.

No comments:

Post a Comment