Mkuu wa Wilaya ya Iramba mkoani Singida, Suleiman Mwenda (katikati) akishiriki kufyatua matofali wakati wa mfululizo wa ziara yake ya kikazi ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo aliyoifanya Kata ya Shelui na Mtoa wilayani humo jana May 29, 2023 akiwa ameongoza na wataalam, watendaji wa Kata na Tarafa pamoja na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama.
Na Mwandishi Wetu, Iramba
MKUU wa Wilaya ya Iramba mkoani Singida, Suleiman
Mwenda amesema atafanya mawasiliano na wahusika wa sekta ya afya ili ziweze
kupatika fedha za kumalizia ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Msai
Kupatikana kwa fedha hizo na kukamilika kwa
ujenzi wa zahanati hiyo kutawaondolea adha wananchi ya kutembea umbali mrefu kwenda
kupata huduma za matibabu maemo mengine.
Mwenda ameyasema hayo wakati alipokuwa kwenye ziara ya kutembelea na
kukagua miradi ya maendeleo katika Kata yaMtoa na Shelui pamojana kusikiliza
kero za wananchi ili kuzitafutia ufumbuzi.
Akiwa katika Zahanati ya Msai inayojengwa kwa
nguvu za wananchi wakisaidiwa na fedha za Mfuko wa Jimbo zinazo simamiwa na
Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi Dkt. Mwigulu Nchemba aliombwa na wananchi
kupatikana kwa fedha za kumalizia ujenzi wa jengo hilo la zahanati hiyo Ili
ianze kutoa huduma na kuwaondolea kero wakazi wa kijiji hicho hasa Wajawazito
na watoto.
"Nimesikia maombi yenu napenda kuwasiliana na
wahusika ili kuwaomba tupate fedha za kumalizia ujenzi wa zahanati iweze
kukamilika na kuanza kutoa huduma haraka iwezekanavyo," alisema Mwenda.
Alisema kijiji hicho ni kikubwa na kuna wananchi
wengi lazima ujenzi wa zahanati hiyo ukamilike haraka ili wananchi wasiendelee
kwenda mbali kupata huduma za afya.
Aidha,Mwenda akiwa kwenye ziara hiyo
aliwasisitiza wasimamizi wa miradi yote inayotekelezwa katika wilaya hiyo
kuhakikisha inakamilika kabla ya June 10,2023.
Katika hatua nyingine Mwenda amewaomba wananchi kuendelea kujitolea nguvu kazi kwa kushirikiana na wataalam na viongozi katika kutekeleza miradi yote inayofadhiliwa na serikali na kuhakikisha inamalizika kwa wakati na viwango kulingana na thamani ya fedha walizozipokea
No comments:
Post a Comment