BWAWA LA MTERA LAFIKIRIWA KUTATUA KERO YA MAJI DODOMA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Saturday, 6 May 2023

BWAWA LA MTERA LAFIKIRIWA KUTATUA KERO YA MAJI DODOMA

 

Kamishna wa Mipango ya Kitaifa, Dkt. Mursal Milanzi, akisalimiana na Mwenyekiti wa Kamati Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira, Mhe. Jackson Kiswaga, wakati wa ziara ya kutembelea Bwawa la Mtera lililopo Mpwapwa Dodoma, ili kuona uwezekano wa kuzalisha zaidi ya lita milioni 133 kwa siku kwa ajili ya kukabiliana na uhaba wa maji katika  jiji la Dodoma.

Kaimu Meneja wa Bwawa la Mtera lililopo Mpwapwa Dodoma, Mhandisi Edmund Seif, akieleza jinsi Maji ya Bwawa hilo yanavyotumika kuzalisha nishati ya umeme, wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya maji na Mazingira, ilipotembelea Bwawa hilo kuangalia uwezekano wa Bwawa hilo kuzalisha maji kwa ajili ya matumizi ya wakazi wa jiji la Dodoma

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), akiaangalia kina cha maji ya Bwawa la Mtera lililopo Mpwapwa Dodoma, wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira, ilipotembelea Bwawa hilo ili kuona uwezekano wa kuzalisha zaidi ya lita milioni 133 kwa siku kwa ajili ya kukabiliana na uhaba wa maji katika  jiji la Dodoma.

No comments:

Post a Comment