𝗪𝗔𝗗𝗔𝗨 𝗪𝗔 𝗘𝗟𝗜𝗠𝗨 𝗪𝗔𝗢𝗡𝗚𝗘𝗭𝗔 𝗠𝗜𝗞𝗔𝗞𝗔𝗧𝗜 𝗞𝗨𝗙𝗔𝗡𝗜𝗞𝗜𝗦𝗛𝗔 𝗘𝗟𝗜𝗠𝗨 𝗬𝗔 𝗟𝗔𝗭𝗜𝗠𝗔 𝟮𝟬𝟮𝟴 - THE HABARII

THE HABARII

HABARI | MATUKIO | MICHEZO.


ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday, 28 September 2026

𝗪𝗔𝗗𝗔𝗨 𝗪𝗔 𝗘𝗟𝗜𝗠𝗨 𝗪𝗔𝗢𝗡𝗚𝗘𝗭𝗔 𝗠𝗜𝗞𝗔𝗞𝗔𝗧𝗜 𝗞𝗨𝗙𝗔𝗡𝗜𝗞𝗜𝗦𝗛𝗔 𝗘𝗟𝗜𝗠𝗨 𝗬𝗔 𝗟𝗔𝗭𝗜𝗠𝗔 𝟮𝟬𝟮𝟴

SERIKALI kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inaendelea kuratibu utekelezaji wa Partnership Compact, mkataba wa pamoja unaowaunganisha wadau wa elimu katika kuhamasisha na kuchangia rasilimali kwa ajili ya kuimarisha sekta ya elimu nchini.


Katika hatua hiyo, wadau wa elimu wamekutana jijini Arusha katika kikao kazi kuanzia Septemba 22 hadi 26, 2026, kwa ajili ya kutathmini utekelezaji wa shughuli za Partnership Compact katika robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2026/27, kubaini hatua zilizofikiwa na kutathmini mchango wa juhudi hizo katika kutekeleza vipaumbele vya Sera ya Elimu na Mafunzo nchini.


Mkutano huo umesisitiza umuhimu wa kuongeza mikakati ya uhamasishaji wa rasilimali ili kuiwezesha Serikali kutekeleza kwa ufanisi mpango wa elimu ya lazima ifikapo mwaka 2028, ambapo makundi rika mawili ya wanafunzi yanatarajiwa kuingia Kidato cha Kwanza.


Kupitia Partnership Compact, Serikali na wadau wa elimu wanaendelea kuunganisha nguvu, utaalamu na rasilimali katika kuunga mkono vipaumbele vya elimu nchini. Ushirikiano huo unalenga kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa mipango ya elimu na kuhakikisha sekta inaendelea kuimarika na kutoa fursa za elimu kwa watoto na vijana nchini.


Wadau wa elimu wakiwa kwenye kikao kazi jijini Arusha. 




Majadiliaano yakiendelea kwenye kikao kazi hicho


Taswira ya kikaao hicho

Majadiliano yaakiendelea


 

No comments:

Post a Comment