TAASISI ya Wakala wa Mabasi yaendayo Haraka (Mwendokasi) –
DART wameungana na Benki ya NMB kupitia kampeni yao inayozidi kushika kasi ya
Upandaji Miti Milioni kwa mwaka 2023, kwa kupanda miti 1,000 aina ya
‘Jacaranda’ katika ushoroba wa Bus Rapid Transit (Mwendokasi).
Zoezi hilo liliongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya DART - Dkt.
Florens Turuka akiambatana, Mkuu wa Wilaya Ubungo - Hashim Abdallah Komba,
Mtendaji Mkuu wa DART Dk. Edwin Mhede na watumishi wa DART.
Kwa upande wa NMB, waliwakilishwa na Afisa Mkuu wa Wateia
Binafsi na Biashara - Filbert Mponzi, Mkaguzi wa Ndani - Benedicto Baragomwa,
Afisa Mkuu wa Technolojia na Mabadiliko ya Kidijitali - Kwame Makundi, Afisa
Mkuu Utekelezaji - Ezekiel Herman pamoja na wafanyakazi kutoka Kanda ya Dar es
Salaam.
Akizungumza katika zoezi hilo, Dkt. Mhede aliishukuru NMB
kwa kuishirikisha DART katika kutekeleza maagizo ya Makamu wa Rais Dkt. Mpango
ya kutaka mamlaka zote za Serikali, taasisi na mashirika ya umma kujikita
katika kampeni hiyo inayolenga kupunguza athari za mabadiliko ya tabia nchi.
“Shukrani NMB kwa wazo bunifu la kuja na kampeni hii, ambayo
kwetu sisi DART ni fursa ya kutuwezesha kurejesha uoto wa asili katika ushoroba
wa barabara zetu, ambao unaondolewa na ujenzi wake. Kampeni hii itatusaidia
kurejesha uhalisia wa maeneo yetu”.
"Tumejipanga kuitunza miti hii, jukumu ambalo
nalikabidhi kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ulinzi wa Miundombinu ya DART
(China-Tanzania Security), El-Malick Aboud, ambaye atashirikiana na watendaji
wa mitaa, kata zinakopita na mradi wa mwendokasi kote Dar es Salaam.
Naye, Mwenyekiti wa Bodi ya Washauri ya DART, Florens
Turuka, aliahidi kuwa miti hiyo 1,000 ambayo wataipanda kuanzia Ubungo kuelekea
Kata za Manzese na Magomeni, wataitunza ipasavyo kama alivyosema Dk. Mhede,
kwani lengo lao DART - ambao wanasafirisha abiria kupitia kauli mbiu ya
'Usafiri wa Umma Nadhifu,' ni kuitunza kwa asilimia 100.





No comments:
Post a Comment