UJENZI NA UKARABATI WA VIVUKO KUTATUA CHANGAMOTO YA USAFIRI KANDA YA ZIWA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday, 28 March 2023

UJENZI NA UKARABATI WA VIVUKO KUTATUA CHANGAMOTO YA USAFIRI KANDA YA ZIWA

 

Muonekano wa awali wa sehemu ya vivuko vinne vinavyojengwa na Kampuni ya Songoro Marine, mkoani Mwanza. Vivuko hivyo ni Kisorya – Rugezi (Ukerewe - Mwanza), Ijinga – Kahangala (Magu - Mwanza), Bwiro – Bukondo (Ukerewe - Mwanza) na Nyakalilo – Kome (Buchosa - Mwanza).

Muonekano wa Kivuko cha MV Misungwi kinachotoa huduma katika eneo la Kigongo na Busisi kikiwa katika matengezo katika yard ya Songoro, mkoani Mwanza.

Kaimu Meneja Vivuko Kanda ya Ziwa na Magharibi Eng. Aloyce Ndunguru, akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi Eng. Godfrey Kasekenya, kuhusu ujenzi wa vivuko vipya vinne, mkoani Mwanza. Vivuko hivyo ni Kisorya – Rugezi (Ukerewe - Mwanza), Ijinga – Kahangala (Magu - Mwanza), Bwiro – Bukondo (Ukerewe - Mwanza) na Nyakalilo – Kome (Buchosa - Mwanza).



Mkurugenzi wa Kampuni ya Songoro Marine, Major Songoro, akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi Eng. Godfrey Kasekenya, kuhusu ujenzi wa vivuko vipya vinne, mkoani Mwanza. Vivuko hivyo ni Kisorya – Rugezi (Ukerewe - Mwanza), Ijinga – Kahangala (Magu - Mwanza), Bwiro – Bukondo (Ukerewe - Mwanza) na Nyakalilo – Kome (Buchosa - Mwanza).

Naibu Waziri wa Ujenzi Eng. Godfrey Kasekenya, akitoa maelekezo kwa Kaimu Meneja Vivuko Kanda ya Ziwa na Magharibi Eng. Aloyce Ndunguru, wakati akikagua utekelezaji wa ujenzi wa miradi ya vivuko vipya na matengenezo ya vivuko katika yard ya Songoro Marine, mkoani Mwanza.

IIMEELEZWA kuwa kukamilika kwa ujenzi wa vivuko vipya vinne na ukarabati wa vivuko vinne vitakavyotoa huduma katika maeneo mbalimbali ya Ziwa Victoria kutapunguza changamoto za usafiri kwa wananchi wanaoishi katika mikoa ya Kanda ya Ziwa na kutarahisisha shughuli za maisha kwa urahisi, uhakika na usalama.


Hayo yamesemwa mkoani Mwanza na Naibu Waziri wa Ujenzi, Eng. Godfrey Kasekenya, wakati alipokagua karakana ya ujenzi wa meli na vivuko ya Songoro na kupata taarifa ya maendeleo ya ujenzi na ukarabati wa vivuko hivyo vitavyogharimu takribani bilioni 26 na kutarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Agosti mwaka huu.


“Nimekagua na nimeridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa vivuko vipya lakini pia na ukarabati wa vivuko unaoendelea, nimatumaini yangu vivuko hivi vitakamilika ndani ya muda kwani kuna baadhi ya maeneo vivuko hivyo havipo au kimebakia kimoja na hivyo kutokidhi mahitaji ya wananchi", amesema Kasekenya.


Amefafanua kuwa kwa sasa ujenzi wa vivuko hivyo unaendelea na vipo katika hatua mbalimbali na kutaja kuwa vivuko hivyo ni Kisorya – Rugezi (Ukerewe - Mwanza), Ijinga – Kahangala (Magu - Mwanza), Bwiro – Bukondo (Ukerewe - Mwanza) na Nyakalilo – Kome (Buchosa - Mwanza).


Aidha, ukarabati wa vivuko unaoendelea ni pamoja na MV Misungwi (Kigongo - Busisi), MV Mara (Iramba - Majita), MV Ujenzi (Kisorya - Rugezi) na MV Nyerere (Bugolora - Ukara).


Aidha, ameiagiza Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), kumsimamia mkandarasi wa Kampuni ya Songoro kufunga vifaa vyote vilivyosanifiwa kuanzia katika hatua za awali hadi vivuko hivyo vitapokamilika.


Naye, Kaimu Meneja Vivuko Kanda ya Ziwa na Magharibi kutoka TEMESA Eng. Aloyce Ndunguru, amesema kuwa wanaendelea na ujenzi wa vituo vipya vitatu ambvyo ni Bwiro (kisiwani) – Bukondo katika Wilaya ya Ukerewe, Kituo ch Ijinga (kisiwani) – Kahangala katika Wilaya ya Magu na Kituo cha Mayenzi – Kanyinya ambapo miradi hiyo ikikamilika itafanya wawe na jumla ya vituo 16 katika kanda hiyo.


Ameeleza pia kanda hiyo ina jumla ya vivuko 17 ambapo kati ya hivyo vivuko vinne vipo katika matengenezo makubwa ambavyo ni MV Misungwi (Kigongo - Busisi), MV Mara (Iramba - Majita), MV Ujenzi (Kisorya - Rugezi) na MV Nyerere (Bugolora - Ukara).


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Songoro Marine, Major Songoro, amemueleza Naibu Waziri huyo kuwa baadhi ya vivuko ambavyo vinafanyiwa ukarabati vipo katika hatua za mwisho za kukalimika na vitarudishwa TEMESA mapema kwa ajili ya kuendelea kutoa huduma.

No comments:

Post a Comment