Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dk.Fatma Mganga (wa pili kulia) akipata maelezo wakati akikagua vifaa mbalimbali vilivyonunuliwa na Serikali kwa ajili ya Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) Mkoa wa Singida kabla ya kufungua kikao cha wadau na karakana mkoani hapa Machi 19, 2023.
Na
Dotto Mwaibale, Singida
KATIBU
Tawala Mkoa wa Singida, Dk.Fatma Mganga
amewataka Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) mkoani hapa kujiendesha
kibiashara ili kuipunguzia mzigo Serikali ambayo imekuwa ikitoa fedha nyingi
kuendesha taasisi hiyo.
Mganga
ambaye alikuwa mgeni rasmi ametoa ombi hilo Machi 29, 2023 wakati akifungua kikao cha wadau na karakana ya Mkoa wa Singida
ambacho pia kilihudhuriwa na Mkurugenzi wa Matengenezo na Huduma za Ufundi
Temesa Makao Makuu Dodoma, Mhandisi Hassan Koronda.
“Tengenezeni magari kwa ubora na weledi
punguzeti gharama za uendeshaji ili muisaidie Serikali na mkimbiliwe na wateja”
alisema Mganga.
Aidha, Mganga aliwataka TEMESA kutumia
fursa waliyonayo kutoka nje kujitangaza ili wafahamike badala ya kukaa tu
ofisini na akaishauri kuanza kutumia TEHAMA kwa ajili ya kupata mrejesho kutoka
kwa wateja wao kupitia ujumbe mfupi.
Mganga alihimiza TEMESA kutoa mafunzo kwa
madereva ya uendeshaji wa magari ili
wajue mbinu ya kuyatunza ukizingatia kuwa ni wadau wao na akaomba waanzishe
kitengo cha uoshaji wa magari ili iwe motisha kwa wateja wanaowapelekea vyombo
vyao vya moto.
Akizungumzia madeni yanayodaiwa na TEMESA
aliomba apewe orodha ya wadaiwa wote zikiwepo Taasisi za Serikali ili aweze
kuonana na wahusika waanze kulipa madeni hayo kwa awamu.
“Serikali inayomatarajio makubwa kuona
mnafanya kazi zenu kwa kuzingatia misingi ya sheria za utumishi wa umma na
kanuni zake kwa kutumia Taaluma zenu kutunza mali za umma hasa magari na
miundombinu ya umeme kwani nagharimu fedha nyingi,” alisema Mganga.
Mkurugenzi wa Matengenezo na Huduma za
Ufundi , Mhandisi Hassan Koronda alisema Serikali imekua ikitenga fedha kila
mwaka na mwaka huu wa fedha wa fedha kiasi cha Sh.Bilioni moja zimetengwa kwa
ajili ya ukarabati wa karakara kumi na mbili katika mikoa mbalimbali ukiwemo
Mkoa wa Singida ambao ujenzi wake wa awamu ya kwanza tayari umekamilika.
Aidha, Koronda alisema Serikali imetoa
kiasi cha fedha Sh.509.8 Milioni kwa ajili ya ununuzi wa vitendea kazi vya
kisasa kwa upande wa umeme, ICT na mitambokwa karakana za mikoa yote Tanzania
kwa lngo la uboreshaji utendaji wa kazi.
Mkuu wa Magari, TEMESA Mkoa wa Singida, Erasto Cheza akitoa
taarifa ya mikakati ya utendaji wa kazi alisema wameyaondoa malalamiko
yaaaaaliyokuwepo awali kwa kuyatambua na kuandaa mikakati ya kuyamaliza kabisa kwa
kushirikiana na wadau wao, mabadiliko ya tabia, matendo na mwenendo kwa kupata
elimu ya kuendana na mahitaji ya wateja.
Cheza alitaja majukumu yao makubwa kuwa ni kufanya matengenezo ya Magari, pikipiki na Mitambo ya Serikali, kufanya matengenezo na Usimikaji wa Mifumo ya Umeme, Mabarafu, viyoyozi na Elektroniki, kufanya matengenezo ya taa za kuongozea magari na taa za barabarani (Street Lights), kutoa ushauri wa Kitaalamu katika nyanja za uhandisi wa Ufundi, Umeme na Elektroniki,kushauri usimikaji wa mifumo mipya ya uhandisi wa Ufundi, Umeme na Elektroniki na kufanya usanifu na usimamizi wa usimikaji wa mifumo ya uhandisi wa Ufundi na Umeme.
No comments:
Post a Comment