JUKWAA LA MAENDELEO YA UTAMADUNI KUSHIRIKIANA KUKUZA UTAMADUNI UCHINI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday, 9 March 2023

JUKWAA LA MAENDELEO YA UTAMADUNI KUSHIRIKIANA KUKUZA UTAMADUNI UCHINI

Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu (kulia) akiteta jambo na Bw. Leo Näscher Naibu Balozi wa Uswisi hapa nchini ambaye pia ni Mkuu wa Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano wa Kimataifa (kushoto) Machi 9, 2023 katika ofisi za Wizara hiyo yenye Makao yake Makuu katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.

Bw. Leo Näscher, Naibu Balozi wa Uswisi hapa nchini ambaye pia ni Mkuu wa Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano wa Kimataifa (kushoto) akifafanua jambo wakati wa kikao na Bw. Saidi Yakubu, Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo (kulia) Machi 9, 2023 katika ofisi za Wizara hiyo yenye Makao yake Makuu katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.

Na Eleuteri Mangi - WUSM, Dodoma

KATIBU Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Balozi wa Uswisi hapa nchini ambaye pia ni Mkuu wa Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano wa Kimataifa Bw. Leo Näscher kuhusu ushirikiano katika eneo la Utamaduni na Sanaa baina ya nchi hizo mbili.

Kikao hicho kimefanyika Machi 9, 2023 katika ofisi za Wizara hiyo yenye Makao yake Makuu katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Bw. Yakubu ameeleza azma ya Serikali katika kusimamia sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo ambazo zinatoa ajira kwa vijana wengi na zina mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi nchini na namna watakavyoshirikiana katika kubadilishana utaalam na uzoefu katika sekta hizo.

Naye Bw. Leo Näscher Naibu Balozi wa Uswisi hapa nchini ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano wa Kimataifa amesema wana Jukwaa la Maendeleo ya Sekta ya Utamaduni (DGP) ambalo linaundwa na Balozi mbalimbali ambapo kwa sasa linaongozwa na Wenyeviti ambao ni Uholanzi na Uswisi wataendelea kushirikiana na Wizara hiyo na watakuwa kiunganishi na wadau mbalimbali wa sekta za Utamaduni na Sanaa wakisaidia katika nyanja za utaalam na ushauri.

No comments:

Post a Comment